Ufunuo 17:8 “Nikamwona yule mwanamke amelewa kwa damu ya watakatifu, na kwa damu ya mashahidi wa Yesu. Nami nikastaajabu ajabu kuu”
Mwanamke katika unabii inawakilisha “kanisa”, Ufunuo 21:2 inasema, “…Yerusalemu mpya…umewekwa tayari, kama bibi-arusi aliyekwisha kupambwa kwa mumewe.” Na Ufunuo 21:9 inasema, “…Njoo huku, nami nitakuonyesha yule Bibi-arusi, mke wa Mwana-Kondoo.”
Hivyo Yohana aliona kanisa ambalo limelewa damu ya watakatifu, na je kanisa hilo ni kanisa gani? Katika fungu la 1 Yohana aliambiwa na malaika kwamba “njoo huku, nitakuonyesha hukumu ya yule kahaba mkuu.” Kahaba huyo, katika fungu la 5 ametajwa kama “mwanamke aliyeketi juu ya mnyama“, -mnyama- katika unabi inawakilisha “ufalme” au “taifa”;
angalia Danieli 7:17
“Wanyama hao…wanne ni wafalme wanne watakaotokea duniani” na Danieli 7:23 “…Huyo mnyama wa nne atakuwa ni ufalme wa nne juu ya dunia…”
Hivyo “mwanamke huyu aliyeketi juu ya mnyama” ni kanisa ambalo lina uwezo wa kidini na kisiasa kwa wakati mmoja (kanisa na serikali). Na Je ni kanisa gani hapa duniani lenye uwezo wa kidini na kisiasa? Ni kanisa la Romani Katoliki pekee! Ambapo kanisa katoliki ni “mwanamke” na Roma ni “mnyama”. Mpaka hapa hakuna haja ya ushahidi zaidi, lakini kwa sababu watu wana mioyo migumu kuamini ngoja tuongeze ushahidi zaidi usioweza kukatalika.
Ufunuo 17:3 inasema, “Akanichukua katika Roho hata jangwani, nikaona MWANAMKE, AMEKETI JUU YA MNYAMA mwekundu sana, mwenye kujaa majina ya makufuru, mwenye vichwa saba na pembe kumi.”
Mnyama huyu anayelichukua kanisa katoliki ana “vichwa 7” na “pembe 10”; hapa vichwa saba vinawakilisha milima saba, Ufunuo 17:9 inasema, “Hapo ndipo penye akili zenye hekima. Vile vichwa saba ni milima saba anayokalia mwanamke huyo.”
Je hapa duniani kuna kanisa na serikali vimekaa juu ya milima saba?
*
Kanisa Katoliki linasema…
“Ni ndani ya mji wa Roma, uitwao Mji wa vilima saba, hivyo eneo lote la Serikali ya Vatican limewekewa mpaka kikamilifu.” –The Catholic Encyclopedia, p 529.
“Je vilima saba vya Roma ni nini?
Roma inajulikana kuwa imejengwa juu ya vilima saba. Roma ilisemwa imepatikana wakati Romulus na Remus, wana mapacha wa Mars, walifika katika futi ya kilima Palatine na wakauanzisha mji, Vilima sita vingine ni Capitoline (kiti cha serikali), Quirinal, Viminal, Esquiline, Caelian, na Aventine.” –Geography.about.com
ENCYCLOPÆDIA BRITANNICA
Vilima saba vya Roma
“…kundi la vilima juu au kuhusu ambapo mji wa Roma wa zamani ulijengwa. Mji wa awali wa Romulus ulijegwa juu ya kilima Palatine (#1) (Kilatini: Mons Palatinus). Vilima vingine ni Capitoline, (#2) Quirinal, (#3) Viminal, (#4) Esquiline, (#5) Caelian, (#6) na Aventine (#7) (Vinavyojulikana kimoja kimoja kwa kilatini kama Mons Capitolinus, Mons Quirinalis, Mons Viminalis, Mons Esquilinus, Mons Caelius, na Mons Aventinus).” –
http://www.britannica.com/seo/s/seven-hills-of-rome/
Hivyo mnyama mwenye vichwa 7 ambavyo ni milima 7 ni ufalme wa Roma, na mwanamke aliyeketi juu ya mnyama huyo au juu ya ile milima 7 ni Kanisa Katoliki. Mpaka hapa hakuna haja ya ushahidi zaidi, lakini ngoja tuongeze ushahidi mwingine labda ndungu watapata kuamini kwa huo.
Ufunuo 17:5 inasema, yule “mwanamke amekaa juu ya mnyama…mwenye pembe kumi“. Pembe katika unabii inawakilisha “mfalme/ufalme” au “taifa”, Danieli akitabiri kuhusu mnyama Roma alisema, “Na habari za zile pembe kumi [za mnyama], katika ufalme huo wataondoka wafalme kumi; na mwingine ataoondoka baada ya hao;…naye atawashusha wafalme watatu” Danieli 7:24.
Hivyo pembe kumi ni wafalme kumi ambao wanatawala katika ufalme huo mmoja wa Roma. Baada ya dola la Roma kuanguka mwaka 476BK liligawanyika katika mataifa/wafalme kumi ambayo ni…
1.Saxon,
kwa sasa ni taifa la Uingereza.
2.Frank,
kwa sasa ni taifa la Ufaransa.
3.Alamanni,
kwa sasa ni taifa la Ujerumani.
4.Visigoth, kwa sasa ni taifa la Uhispania.
5.Suevi, kwa sasa ni taifa la Ureno.
6.Lombard,
kwa sasa ni taifa la Italia.
7.Burgundia,
kwa sasa ni taifa la Uswidi.8Heruli,
liling’olewa na pembe ndogo 493 B.K.
9Vandal, liling’olewa na pembe ndogo 534 B.K.
10.Ostrogoth,
liling’olewa na pembe ndogo 538 B.K.
Hizo ndio pembe kumi za mnyama Roma, Unabii katika Danieli 7:8 na 24 unasema kuwa, baada ya pembe hizo kumi ambazo ni wafalme kumi wa dola la Roma, kati yao ingetokea pembe nyingine ndogo ambayo ni mfalme mwingine, ambaye ni Uapa wa Vatikani; nao ungelikuwa tofauti na wale wafalme 10 kwa sababu una nguvu za kidini na kiserikali tofauti na wale 10. Pia pembe ndogo ambaye ni Upapa angezing’oa pembe 3 katika zile pembe 10 za mnyama Roma.
Baada ya kanisa katoliki kupitisha fundisho la utatu katika baraza la 2 huko Konstantinapoli mwaka 381bk, baraza liliamuru kwamba wote wasiokubaliana na imani ya utatu waangamizwe; hivyo mataifa ya Waario (Arians); watu ambao hawakuamini fundisho la utatu, mataifa yao matatu; Heluli, Vandalis, na Ostrogoth yaliangushwa na kanisa Katoliki. Hivyo Upapa ulizing’oa kabisa pembe hizo 3 kama Danieli alivyotabiri, na mataifa 7 yaliyobaki leo yanaitwa Umoja wa Ulaya [EU].
Hivyo yule mnyama mwenye pembe kumi na vichwa saba ambavyo ni milima 7 ni ufalme wa Roma, na yule mwanamke aliyeketi juu yake ni Kanisa Katoliki. Na hivyo yule mwanamke wa Ufunuo 17:6 “amelewa kwa damu ya watakatifu, na kwa damu ya mashahidi wa Yesu…” ni kanisa Katoliki lenyewe. Je historia inathibitisha kuwa kanisa Katoliki liliwahi kumwaga damu ya watakatifu na mashahidi wa Yesu?
“Kwa sababu ya kufundisha imani kinyume na mafundisho ya Roma, historia inaonyesha vifo vya wafia dini zaidi ya milioni 100” –Brief Bible Readings, p 16.
Kanisa Katoliki linasema…
“Katoliki ana baadhi ya sababu kwa upande wake wakati anapotoa adhabu kwa waasi wa kidini, kwa maana anajidaia jina la Ukristo kwake mwenyewe kwa kuzuia, na anajidai kufundisha kwamba uwepo wa Roho wa Mungu kamwe hautaondoka kwake…Siyo kosa zaidi kumuua mtu kwa sababu ya uasi wa kidini, kuliko kwa sababu ya uuaji,…[na] katika mambo mengi mateso kwa maoni ya kidini siyo tu kwamba yanaruhusiwa, lakini ni ya busara na ya lazima.” –The Lawfulnees of Persecution” in the Rambler, 4, June, 1849, pp 119, 126. (“The Rambler” lilikuwa ni gazeti la kila siku la Romani Katoliki lililochapishwa kuanzia mwaka 1848 hadi 1862).
“Chini ya mawazo na desturi za kijerumani, mateso yalitumiwa kidogo kuanzia karne ya 9 hadi karne ya 12, lakini kwa uhuikaji wa sheria ya Romani mateso yalianzishwa tena katika karne ya 12…Katika mwaka 1252 (Papa) Innocent IV aliruhusu adhabu ya mateso juu ya waasi wa kidini kwa kutumia mamlaka ya kiserikali, na mateso yakaja kuwa na mahali palipojulikana katika utaribu wa mahakama ya kiuchunguzi.” –New Catholic Encyclopedia, arts. “Inquisition”, “Auto-da-Fe’,” na “Massacre of St Bartholomew’s Day.”
BWANA AWAITA WOTE WALIOPO KWA HUYU MNYAMA WATOKE HARAKA SANA
YHWH IS GOOD
Sent using
Jamii Forums mobile app