'Vestiges' kwenye miili ya wanyama, ushahidi tosha kwamba hatukuumbwa, bali tuli-'evolve' kuwa tulivyo

Nadharia ya evolution bado changa na haijitoshelezi.
Kwa mfano tendo la kuzaa ni la uchungu sana, sasa evolution kwa nini usifanye kazi yake?
Pengine angalau tutage tuatamie kama kuku.
Toto la kilo sita la nini?
Umeshawahi kumuona kuku akitaga? Na unadhani hana maumivu mkuu??

Halafu nadhani umepotoka. Yaani evolution haipo kwasababu ya kuongeza "comfort ability " ila ipo kwa vitu ambavyo havina matumizi. Yaani ni njia ya kucope Na mazingira. Inalazimu mwili ujibadilishe. Sasa mwili wa mwanamke tayari una hormones ambazo zinawezesha kuzaa kuwezekane kwahiyo sidhani kama mfano wako ni sahihi.

Japokua kuna mifano ambayo wanasayansi wanaitumia ambapo evolution imefeli Na ni kweli hii nadharia haijakamilika hapo nakubaliana na wewe

Ila nikiangalia mifano kama ya jinsi binadamu wenye manyoya wanapungua (kuvaa nguo) na pia jinsi teknolojia inavyotufanya kuwa wavivu (misuli mingi haina umuhimu) nk nk naona kabisa kuna upande evolution inaleta mantiki
 
Sasa kichwani nywele na mavuzi ya nini kuna baridi wapi?
Kichwani kwapani mapajani nywele za kazi gani?
Kichwani zipo kwa kazi nyingine (zaidi ya ile kuzuia baridi ) ndomaana zimebaki mpk leo,kope, nyusi kuzuia jasho lisiingie machoni mavuzi (kuzuia friction)yaani yalikua na kazi ya ziada ndomaana yapo mpk leo
 
Nikuulize maswali mawili

1.Nipe tofauti kati ya adaptation na evolution
2.Ni misuli ipi hiyo ambayo toka teknolojia imekuwa basi yenyewe haina kazi?
 
Nikuulize maswali mawili

1.Nipe tofauti kati ya adaptation na evolution
Ngoja nikuelezee lugha rahisi adaptation ni mabadiliko ya muda mfupi ili kuwezesha kiumbe kusurvive. Mfano tajiri aliyezoea kuishi kwenye jumba la kifahari na watumishi akipelekwa jangwani aishi pekeyake hawezi kwenda kule akawa analala tu mpk saa5 asubuhi. Hata survive.Ataadapt na maisha hayo mapya. Kwa muda mrefu kizazi chake kinaweza hadi kubadilika kupata maumbile mapya ya kupambana na jua kali na ukame nk. Hiyo ndo evolution.Au tukisema evolution (Ina micro evolution na macro evolution ) basi Micro evolution=adaptation

Mfano mwingine unaona hii picha inaitwa evolution of Coca-Cola

Ila humo ndani kuna kipindi ambacho kampuni ya Coca-Cola walibadilisha bei labda (kutokana na great depression ) au ladha kidogo nk. Hiyo ni adaptation kufuata nguvu ya wqnunuaji
 
2.Ni misuli ipi hiyo ambayo toka teknolojia imekuwa basi yenyewe haina kazi?
Naomba nikujibu tena kwa mfano. Zamani binadamu walikua na uwezo wa kusafiri kwa kutembea kutoka Kongo mpaka bagamoyo na mizigo juu. Wakina mama walikua wanakoboa mahindi kwa kinu na kusaga kwa mawe. Jamii za wawindaji walikua wanauwezo wa kuzunguka swala na kumbananisha mpaka wanamkamata kwaajili ya nyama. Baadae teknolojia ikaleta mitego,mishale ya sumu,magari,mashine za kusaga nk. Kwahiyo muda unavyokwenda tunajikuta hatutumii kazi za msuli tunatumia mashine kutoka babu zetu labda inakuja kwetu mpk kwa wajukuu wetu. Pengine mwaka 2100 kutakua na mjukuu wako ambaye toka amezaliwa mpk anakufa hajawahi kutembea km 100 au kubeba mizigo wa kg50 inapoendelea hivyo vizazi vinavyofuata hawawezi kuwa na uwezo wa msuli kama tuliokua nao sisi. Genetics zenyewe zinachagua kuwa hiki kitu sio muhimu tena kizazi hiki
 
Good then why mbuni wabaki kama walivyo hali ya kuwa pamepita changes nyingi since age ya dinosaurs?
 
Kuna haja gani kuzaana kuwepo ilihali vitu vinatokana na evolution?
achana na ujinga wa kizungu
Eti miaka milioni 200
Chukulia tu miaka 100 iliyopita ,ongezeko la watu kwa miaka hiyo, maendeleo ya technolojia kwa miaka hiyo 100 ,halafu uassume miaka milioni
Think out of the box
za kuambiwa changanya na zako
 
Reactions: Cyb
Good then why mbuni wabaki kama walivyo hali ya kuwa pamepita changes nyingi since age ya dinosaurs?
Sio lazima kubadilika ila hata hivyo sidhani kama wanabaki walivyo tu mkuu. Ukizingatia haya mambo yanakwenda kwa vizazi. Yani sio kama vile Leo utawaona wana manyoya halafu kesho hawana. Mara nyingi ni swala la miaka 200+
 
😂😂😂😂😂 Inaonekana hauna info nyingi mkuu nikupe kwanza homework hebu fuatilia jinsi xoxa wanavyowinda, halafu uniambie je? yule actor wa "Gods must be crazy" kwa jina la Nǃxau ǂToma au tumezoea kumuita msandawe.
je ? familia yake itakuwa haiwezi kuwinda kwa sababu baba yao aliiishi maisha tofauti na uwindaji kwa muda mrefu?

Bado hiyo theory yako haija prove hiyo misuli kwanini haifanyi kazi , ila jibu lipo kwenye temporary adaptation means tunapo change mazingira basi miili yetu inafanya temporary changes ili iendane na mazingira husika kwa muda husika na kama utahama hayo mazingira means mwili utafanya changes tena.
 
Sasa kichwani nywele na mavuzi ya nini kuna baridi wapi?
Kichwani kwapani mapajani nywele za kazi gani?
Most likely aina na mahali ya nywele zilipo ni kutokana aesthetics preferences za opposite sex pamoja na functional adaptation, mfano vichwa vilivyokuwa na nywele viliweza kukingwa na jua kali na hivyo ubongo ukawa unakua vizuri na wakafanikiwa zaidi kwa kutumia akili zao, na wengine wakapotea kwa salectiva adaptation ya mazingira. Na kwa muonekano, leo tukiwa mwanamke mwenye nywele vipilipilo na mwenye nywele ndefu kaini curly za kujikunja kunja, wanaume wote watapambana kuzaa nae , halikadhalika kwa watoto atakaowazaa, watagombaniwa kama mpira wa kona, yule mwenye vipili pili atapewa mimba kama kuonewa huruma tu, atazalishwa kitoto kimoja kususiwa akilee mwenyewe, baada ya miaka 1000 jamii yote itakuwa na watoto wenye nywele ndefu, laini za kujikunja, hiyo ndio evolution, its real and logical ( ina mantiki).
 
swala la mtu kuumbwa ni uongo wakizamani sana na ni aibu hata kuendelea kuwafundisha watoto zetu
 
Sio lazima kubadilika ila hata hivyo sidhani kama wanabaki walivyo tu mkuu. Ukizingatia haya mambo yanakwenda kwa vizazi. Yani sio kama vile Leo utawaona wana manyoya halafu kesho hawana. Mara nyingi ni swala la miaka 200+
unajua kuwa mbuni wame exist since dinosaurs wakiwepo na dinosaurs walikuwepo kabla ya evolution ya binadamu (kutokana na theory ya evolution) means binadamu kama tunavyojulikana tumetokea miaka 65 million na zaidi baada ya dinosaurs kutoweka (volcanic eruptions na asteroids you know the story.)

swali ni WHY MBUNI WABAKI KAMA WALIVYO NA HALI YA KUWA WAME EXIST SINCE DINOSAURS AGE NA WAKA SURVIVE DESTRUCTION?
 
swala la mtu kuumbwa ni uongo wakizamani sana na ni aibu hata kuendelea kuwafundisha watoto zetu
Hauwezi uka prove kwamba hatujaumbwa kama unaweza i dare you mkuu.
 
Hauwezi uka prove kwamba hatujaumbwa kama unaweza i dare you mkuu.
Ni kweli siwezi kwasababu hakuna uthibitisho unaopimika na kuthibitisha kua watu waliumbwa.

Vipi unao uthibitisho kuonesha watu waliumbwa?
 
Msandawe anawinda halafu ashindwe kuwinda? Sijaelewa

Hapo sehem ya pili umeongelea adaptation nimekuelezea inavyofanya kazi na jinsi pia evolution inavyofanya kazi

Okey kama kwa mfano wako huo turudi nyuma kwamba tukianza kukaa nje wala moto hakuna tutaota manyoya tena? Sijui kama nakuelewa ndugu
 
Nimekujibu pia evolution theory sio lazima mbona huelewi? Sio law ni theory ambayo inachagua kutokana na nature ya kila kiumbe. Sio kama gravity kwamba kikienda juu lazima kurudi Chini

Inawezekana sina taarifa za kutosha wewe sema kwanini habadiliki? Ninachangia kwa jinsi ninavyofahamu mkuu kwa jinsi nilivyosoma na ninayoyaona field (Geo ) ila haimanishi mimi najua kila kitu
 
Yaani nashangaa kuna watu wanashindwa kuelewa logic ndogo tu hii ya chain za evolution zinavyokwenda. Anadhani kwamba ni swala la miaka 10 nyani wanakua binadamu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…