KERO VETA Chang'ombe na changamoto ya kuchelewa kutolewa kwa matokeo ya kozi ya udereva wa malori (HGV) – Intake ya 16, Temeke

KERO VETA Chang'ombe na changamoto ya kuchelewa kutolewa kwa matokeo ya kozi ya udereva wa malori (HGV) – Intake ya 16, Temeke

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Wakuu, mimi pamoja na wenzangu tulijiunga na kozi ya udereva wa malori katika kituo cha Temeke mwezi Julai na kumaliza mwishoni mwa Agosti. Tulikuwa kundi la 16 (Intake 16).

Cha kushangaza, hadi sasa matokeo yetu hayajatoka, na hatujui hatma yetu. Hali hii inatupa wasiwasi, hasa kwa baadhi yetu ambao leseni zao zinakaribia kuisha muda wake.

Pia, kuna uwezekano baadhi yetu tukafeli na kuhitaji kurudia mtihani, jambo litakaloongeza muda zaidi wa kusubiri. Hivyo, tunajiuliza: Je, kozi ya mwezi mmoja inapaswa kuchukua karibu mwaka mzima bila hata matokeo kutolewa?

Kinachotushangaza zaidi ni kwamba wanafunzi waliojiunga baada yetu tayari wamepata matokeo yao. Wanafunzi wa kozi za Basic, PSV na hata HGV wa Intake ya 17 matokeo yao yameshatoka, lakini sisi wa Intake ya 16 bado tunaendelea kusubiri bila maelezo ya kuridhisha.

Tunaomba uongozi wa kituo husika utupe ufafanuzi kuhusu sababu za kuchelewa kwa matokeo yetu na lini yanatarajiwa kutolewa.

Ikiwa matokeo pekee yanachukua muda wote huu, je, tutasubiri kwa muda gani kupata vyeti vyetu?

Tunaiomba mamlaka husika ilifanyie kazi suala hili ili wanafunzi wapate matokeo yao kwa wakati na waweze kuendelea na mipango yao ya kazi bila vikwazo visivyo vya lazima.
 
Back
Top Bottom