KERO VETA Mbeya kuna shida gani? Tumemaliza mafunzo ila mchakato wa kukamilisha mafunzo unasuasua

KERO VETA Mbeya kuna shida gani? Tumemaliza mafunzo ila mchakato wa kukamilisha mafunzo unasuasua

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Mimi ni mmoja wa waathirika wa ukosefu wa ajira rasmi serikalini tangu nilipohitimu chuo miaka 10 iliyopita. Kutokana na hali hiyo, nilijiongeza kwa kujifunza taaluma nyingine yenye masharti tofauti na taaluma yangu ya awali ili niweze kujipatia kipato.

Katika kutekeleza majukumu yangu katika taaluma hiyo, nilitakiwa kuhudhuria kozi fupi ya kuhuisha leseni yangu ya udereva. Nilichagua VETA Mbeya kutokana na urahisi wa kufika chuoni hapo bila kutumia gharama kubwa.

Hata hivyo, tangu tulipomaliza kozi hiyo, sasa ni karibu miezi miwili lakini mchakato wa kukamilisha mafunzo na taratibu zinazofuata bado haujakamilika.

Kwa mujibu wa utaratibu uliopo, dereva anayehitaji kuhuisha leseni anatakiwa kuhudhuria mafunzo katika chuo kinachotambuliwa na Serikali, kisha kufanya mtihani unaosimamiwa na Jeshi la Polisi, ambao unahusisha mtihani wa vitendo barabarani pamoja na wa maandishi. Matokeo ya mtihani wa Polisi pamoja na cheti cha chuo huingizwa kwenye mfumo wa Jeshi la Polisi, hatua inayomwezesha dereva kuhuisha leseni yake popote nchini.

Kinachotutia wasiwasi zaidi ni kwamba si sisi tuliomaliza mafunzo miezi miwili iliyopita pekee ambao tunasubiri. Baadhi ya madereva waliomaliza mafunzo katika VETA Mbeya miezi mitatu hadi minne iliyopita bado hawajaitwa kufanya mtihani wa Polisi ili waweze kuendelea na mchakato wa kuhuisha leseni zao.

Kilio chetu ni kwamba ikiwa kuna changamoto ya mfumo wa kitaifa, tungeelewa. Hata hivyo, taarifa tulizonazo zinaonyesha kuwa madereva waliosoma kozi hiyo hiyo katika vyuo vingine vya VETA wamekamilisha mafunzo, wamefanya mtihani wa Polisi na wamepatiwa vyeti.

Kwa nini hali hii ipo VETA Mbeya pekee? Kuna changamoto gani inayozuia kukamilishwa kwa mchakato huu?

Ikiwa kuna tatizo au changamoto inayosababisha kuchelewa, tunaomba wahusika watuambie ukweli ili tujue hatua za kuchukua. Kuendelea kusubiri bila taarifa kunawaweka madereva wengi katika hali ngumu, hasa kwa kuwa leseni ni sehemu muhimu ya ajira na kipato chao.

Kuna malalamiko mengi kutoka kwa madereva kuhusu suala hili. Tunaomba mamlaka husika zilichunguze na kusaidia kutatua changamoto hii ili madereva waliokamilisha mafunzo waweze kufanya mtihani wa Polisi na kuhuisha leseni zao kwa wakati.

Tunaomba sauti yetu isikike na suala hili lifanyiwe kazi.
 
Mimi ni fundi wa rangi yani fundi haswa ila sijasoma VETA na ninahitaji kuwa na cheti cha VETA nifanye mchakato gani ili niwe nacho
 
Suluhisho, ni hizo pande mbili wakae na wafanye maamuzi ni lini mtihani wa kuwapima ufanyike.
 
Back
Top Bottom