VETA yatangaza mpango wa kuzalisha simu brand name 'Ujuzi pro

VETA yatangaza mpango wa kuzalisha simu brand name 'Ujuzi pro

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
2,318
Reaction score
4,079
Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) imetangaza mpango wake wa kuanza kuzalisha na kuunganisha simu janja nchini chini ya chapa inayojulikana kama "Ujuzi Pro". Mkurugenzi Mkuu wa VETA, CPA Anthony Kasore, ameeleza kuwa utengenezaji wa simu hizo hapa nchini ni hatua kubwa ya kimkakati inayolenga kuongeza ujuzi wa kiteknolojia na kukuza sekta ya viwanda nchini Tanzania.

CPA Kasore amethibitisha kuwa mchakato huo umefikia hatua nzuri baada ya kupata vibali vinavyohitajika kutoka mamlaka za udhibiti ikiwemo Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) na Tume ya Ushindani (FCC).

Ameeleza kwa sasa VETA iko kwenye hatua za mwisho za kukamilisha taratibu za kupata namba za utambulisho wa vifaa vya mawasiliano (IMEI) ili simu hizo ziweze kuingia sokoni rasmi.

Je, upo tayari kutumia simu iliyotengenezwa na VETA?


 
Sawa, ngoja tuone jinsi itakavyokuwa wakati hizo simu zikishindania soko la teknolojia ya mawasiliano.
 
Njia nyepesi ni kufanya kama Kipanya. Unaenda China, unatafuta watengenezaji wa simu zisizo na brand, unanunua kwa jumla, unawapa brand Yako waweke.
Sisi hatuna Tu umoja ila Nchi nyingi Duniani ambazo zina watu wengi wanalazimisha assembling ifanyike kwao,

Assembling ni kuunga Tu motherboard, speaker, kioo na vifaa vingine, kama fundi mtaani anafungua simu, kubadili kifaa na kufunga ikafanya KAZI kwanini assembling ishindikane?

Tunaweza tukakaa Nchi zote zinazoongea Kiswahili kudemand assembling ya simu ifanyike nyumbani kwa Asilimia Fulani.
 
Ku assemble simu si Kazi, ni kitu kinawezekana kabisa, pia hongera Yao kuweka wazi Wana assemble badala ya kutumia siasa za kuanza kuclaim gunduzi za watu.

Waache wa assemble Ajira zitaongezeka.
Wanataka credit hapo kwamba wameunda simu. Bora tukomae na kuassemble, itakua na faida nyingi sana ikiwemo upatikanaji wa spare original.
 
Product zetu kwa nini huwa tuna zi localize especially branding kwenye tech.?
Hatufikiri nje ya soko la Tanzania/Africa, mfano jina la hiyo simu ‘ujuzi pro’ hii ni kudumaza product visibility katika soko kubwa.
Mfano hata leo tukitengeneza LLM utasikia inaitwa Swahili/Bongo AI.

Naamini hata kama whatsapp, facebook, weChat kama vinge vumbuliwa bongo bado vingepewa majina yenye kuvipa mipaka ya kufikia soko kubwa.

Haijalishi ni kwa kiasi gani tunataka kujinasibisha na bidhaa ni wakati wa kufikiri kuhusu majina ya hizo bidhaa za kiteknolojia.
 
Mkuu nakuelewa hoja yako ila kuna suala la ubora, sidhani kama ufundi na ujuzi wa bongo unaweza kushindana kimataifa. Lakini pia kuna suala la kuthamini lugha ya taifa japo binafsi sipendi na huwa naudhika sana kuona maneno ya kiswahili kwenye tech.

Kuna wadau walitengeneza language inaitwa Nuru nilipoona tu syntax na semantic rules zake nikapoteza interest kabisa kuna vitu kama andika() sijui jaza() 😁🙌
Mfano;
arr = []
sukuma(arr, 2)

au

jumlisha = unda(x, y) {
rudisha x + y
}
andika(jumlisha(3,4))

Kuna kitu kinapotea ukiweka kiswahili kwenye mambo kama haya
Ujuzi wa bongo kushindana kimataifa mbona hilo kwa sasa lipo na linafanyika.

Ila kwa Hawa wanao translate compilers na programming languanges huwa naona wanapoteza muda tu. Badala ya kuandika Context nikaandike muktadha hili halijakaa sawa kabisa
 
Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) imetangaza mpango wake wa kuanza kuzalisha na kuunganisha simu janja nchini chini ya chapa inayojulikana kama "Ujuzi Pro". Mkurugenzi Mkuu wa VETA, CPA Anthony Kasore, ameeleza kuwa utengenezaji wa simu hizo hapa nchini ni hatua kubwa ya kimkakati inayolenga kuongeza ujuzi wa kiteknolojia na kukuza sekta ya viwanda nchini Tanzania.

CPA Kasore amethibitisha kuwa mchakato huo umefikia hatua nzuri baada ya kupata vibali vinavyohitajika kutoka mamlaka za udhibiti ikiwemo Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) na Tume ya Ushindani (FCC).

Ameeleza kwa sasa VETA iko kwenye hatua za mwisho za kukamilisha taratibu za kupata namba za utambulisho wa vifaa vya mawasiliano (IMEI) ili simu hizo ziweze kuingia sokoni rasmi.

Je, upo tayari kutumia simu iliyotengenezwa na VETA?

Utakuta kila component imekuwa designed na produced in china wewe ni kupachika jina kama ilivuokuwa kwa trump phone
 
Back
Top Bottom