Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) imetangaza mpango wake wa kuanza kuzalisha na kuunganisha simu janja nchini chini ya chapa inayojulikana kama "Ujuzi Pro". Mkurugenzi Mkuu wa VETA, CPA Anthony Kasore, ameeleza kuwa utengenezaji wa simu hizo hapa nchini ni hatua kubwa ya kimkakati inayolenga kuongeza ujuzi wa kiteknolojia na kukuza sekta ya viwanda nchini Tanzania.
CPA Kasore amethibitisha kuwa mchakato huo umefikia hatua nzuri baada ya kupata vibali vinavyohitajika kutoka mamlaka za udhibiti ikiwemo Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) na Tume ya Ushindani (FCC).
Ameeleza kwa sasa VETA iko kwenye hatua za mwisho za kukamilisha taratibu za kupata namba za utambulisho wa vifaa vya mawasiliano (IMEI) ili simu hizo ziweze kuingia sokoni rasmi.
Je, upo tayari kutumia simu iliyotengenezwa na VETA?