Viagra haitibu upungufu nguvu za kiume -daktari

Viagra haitibu upungufu nguvu za kiume -daktari

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
42,872
Reaction score
34,363
g-hlt-110209-viagra-12p.jpg




VIAGRA na tiba zinazotolewa na waganga wa kienyeji , haziwezi kutibu tatizo la upungufu wa nguvu za kiume, kwa kuwa upungufu huo ni wa kisaikolojia.
Mganga wa mradi wa uhamasishaji wa ushiriki wa wanaume katika afya ya uzazi na jinsia

mkoani Rukwa , Dk John Komba alibainisha hayo katika semina ya siku moja.
Semina hiyo iliwajumuisha waandishi 15 kutoka Klabu ya Waandishi wa Habari mkoani Rukwa. Ilifanyika mjini hapa jana.Alibainisha asilimia 60 ya wanaume walio na upungufu

huo ni wa kisaikolojia wakati asilimia 40 ya wanaume hao ni wale wanaosumbuliwa na magonjwa ya kisukari na shinikizo la damu.
Alisema tatizo kubwa linalowakabili wanaume hao wenye dosari hizo ni kuogopa kwenda hospitalini na katika vituo vya

kutolea huduma za afya kutibiwa.
Badala yake, wanaamua kutumia tena kwa siri dawa za kienyeji na pia Viagra, kwa sababu tu hawataki kuwa wazi na kuzungumza na wenza wao.Dk Komba alisema sehemu kubwa ya matatizo hayo ya kiafya ya mfumo wa

uzazi kwa wanaume ni ya kisaikolojia , hali mbaya ya kiuchumi mahusiano mabaya na wenza wao na ugomvi wa kifamilia.
Alisema vitu vyote hivyo husababisha wanaume wengi kuwa na msongo wa mawazo hivyo kujikuta wakisumbuliwa na

upungufu wa nguvu za kiume.
Alibainisha kuwa ili wanaume hao waondokane na matatizo hayo lazima wawe na afya nzuri ambayo itasababisha utulivu wa akili, itaboresha mahusiano baina ya wenza na imani ya kiroho.Dosari yoyote itakayosababisha kutokuwepo kwa utulivu wa akili itamfanya mtu kuwa na msongo wa mawazo hivyo hatakuwa na afya njema," alisisitiza .http://www.habarileo.co.tz/index.ph...iagra-haitibu-upungufu-nguvu-za-kiume-daktari
 
Dah ni kweli...so hata yule kiongozi mashuhuri alifariki Kenya yule 2 months ago ,Rais mnigeria yule they all had psychological(stress) condition!!-Na kizazi hiki cha kupiga masterbation sana ,itabd nijipange tu nianzishe mradi wa kuwauzia mikuyati mana after 10 years mideki yao itakuwa imechokaa.....(I expect viagra,mikuyati market after 10 years to expand massively)

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Hata mie namshangaa huyo MSEMISHAJI? Naona alikosa mada ilihali kesha vuta mkwanja wa Semina.

Watu wengi wanajua hivo mkuu so hakufanya vibaya he was making things clear

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Kunde za.....ni dawa ya kuongeza nguvu za kiume.
 
Back
Top Bottom