Herbalist Dr MziziMkavu
JF-Expert Member
- Feb 3, 2009
- 42,872
- 34,363
VIAGRA na tiba zinazotolewa na waganga wa kienyeji , haziwezi kutibu tatizo la upungufu wa nguvu za kiume, kwa kuwa upungufu huo ni wa kisaikolojia.Mganga wa mradi wa uhamasishaji wa ushiriki wa wanaume katika afya ya uzazi na jinsia
mkoani Rukwa , Dk John Komba alibainisha hayo katika semina ya siku moja.Semina hiyo iliwajumuisha waandishi 15 kutoka Klabu ya Waandishi wa Habari mkoani Rukwa. Ilifanyika mjini hapa jana.Alibainisha asilimia 60 ya wanaume walio na upungufu
huo ni wa kisaikolojia wakati asilimia 40 ya wanaume hao ni wale wanaosumbuliwa na magonjwa ya kisukari na shinikizo la damu.Alisema tatizo kubwa linalowakabili wanaume hao wenye dosari hizo ni kuogopa kwenda hospitalini na katika vituo vya
kutolea huduma za afya kutibiwa.Badala yake, wanaamua kutumia tena kwa siri dawa za kienyeji na pia Viagra, kwa sababu tu hawataki kuwa wazi na kuzungumza na wenza wao.Dk Komba alisema sehemu kubwa ya matatizo hayo ya kiafya ya mfumo wa
uzazi kwa wanaume ni ya kisaikolojia , hali mbaya ya kiuchumi mahusiano mabaya na wenza wao na ugomvi wa kifamilia.Alisema vitu vyote hivyo husababisha wanaume wengi kuwa na msongo wa mawazo hivyo kujikuta wakisumbuliwa na
upungufu wa nguvu za kiume.Alibainisha kuwa ili wanaume hao waondokane na matatizo hayo lazima wawe na afya nzuri ambayo itasababisha utulivu wa akili, itaboresha mahusiano baina ya wenza na imani ya kiroho.Dosari yoyote itakayosababisha kutokuwepo kwa utulivu wa akili itamfanya mtu kuwa na msongo wa mawazo hivyo hatakuwa na afya njema," alisisitiza .http://www.habarileo.co.tz/index.ph...iagra-haitibu-upungufu-nguvu-za-kiume-daktari