Kididimo
JF-Expert Member
- Sep 20, 2016
- 4,153
- 3,800
Mimi binafsi nimetembelea vituo kadhaa vya BBT kwa upande wa Unenepeshaji mifugo kwa lengo la kujifunza. Vikiwemo Kikulula- Karagwe,Mabuki- Mwanza nk. Nimegundua yafuatayo;
1. Vijana wengi waliochaguliwa kushiriki BBT wamekata tamaa . Walichoitiwa sicho walichokikuta. Wameongezewa muda wa kukaa zaidi makambini bila kushirikishwa.
2. Ngombe walitakiwa kunenepeshwa kwa batch 4 kwa mwaka, hadi mwaka unaishilia , hata batch ya kwanza haijamalizika kufika sokoni. Imeonekana ngombe wao hawana sifa za soko, hivyo hakuna mnunuzi wa uhakika.
3. Ngombe walionunuliwa kwa unenepeshaji, hawatunzwi kwa kanuni za ulishaji vyakula vya ziada. Wanachungwa kama wa wanavijiji . Wamekaa karibia mwaka na hawajabadilika uzito.
4. Nilichokigundua ni kama zoezi lilianza bila maandalizi ya kutosha. Nafikiri Kuna watu wanahitajika kuwajibika kwa udanganyifu huo.
5. Inasemekana, hata ile ahadi ya Raisi kumpa kila kijana mtaji wa kununua ngombe 10,anenepeshe kwa mzunguko wa miezi mitatu mitatu,faida iwe yake haipo tena. Hakuna utaratibu wala kumbukumbu za wazi . Vijana wameshaelekezwa wakakope Benki.
Nimeyaeleza haya kwa lengo la kujenga. Vijana hawa ni Taifa la kesho. Tunapowapa ahadi kwa lengo la kuwaandalia ajira ni vyema tutimize yaliyokubaliwa.
Je, Mh. Raisi na Mama yetu, ndivyo hivi alivyotaka? Au kuna watu wanataka kumuangusha au kumchonganisha na vijana wetu?