Rais Mama Samia Suluhu Hassan hapaswi kuvaa viatu au kutembelea kivuli cha Mwendazake Hayati JPM.
Mzee Ruksa hakutembelea kivuli cha Mwl Nyerere,Marehemu Mzee Mkapa hakutembelea kivuli cha Mzee Ruksa vile vile Mzee wa Msoga hakutembelea kivuli cha Mkapa.
Ikiwa wengi hawakutembelea vivuli vya watangulizi wao kwanini Rais Mama Samia atembelee kivuli cha mwendazake.
Rais Mama Samia kumuhimiza au kumtaka kwa namna yoyote atende kama mtangulizi wake kwa maoni yangu mimi ni kumkosea heshima.Yaani mnataka Mama naye aanze kubambika kesi,atudanganye ATCL inatoa gawio kumbe mihasara kibao,au na yeye ajenge Chake Chake International Airport ndio muone kafanana na Magufuli.Enzi za Magufuli zimepita kama ziluvyopita enzi za Mwl Nyerere.Tuondolee uchuro wa Magufuli utawala wake ulimalizika Rais Mama Samia alipakula kiapo.