Mtoto wa Shule
JF-Expert Member
- Nov 16, 2014
- 15,133
- 11,914
Kinyungu, Kinyungu. Naomba ujue ya kwamba, mapenzi yangu kwa JPM are "untainted".Yaani leo ww leo ndiyo wa kusema hii nchi siyo ya watu fulani peke yao? Kweli mwendazake alikuwa na mashabiki wazandiki
Umenena vyema sana🙏🙏 Swala hapa sio kuvaa au kuvua viatu vya mtu, au kuwa na image ya mtu mwingine as long as Yule Ni JPM na huyu ni SSH, cha msingi ni uongozi ambao unafata sheria na kanuni zake, utawala wa kijamii unaozingatia haki ya kila mwana jamii, unaotambua wajibu wake, unaotambua tofauti mbali mbali zilizo kwenye jamii na kuweza kuleta pamoja jamii hiyo na kuwa kitu kimoja kama taifa lenye msukumo wa dhati wa kujenga nchi.Ataheshimiwa Atapongezwa Atahukumiwa kutokana na namna ataliongoza Taifa
Kuondoa makandokando
Kuondoa Ukabila
Kuondoa Udini
Kuondoa Hofu
Haki kwa kila Mtz
Kuupinga Ubadhirifu wa mali za Umma (miradi mikubwa ni moja ya Ubadhirifu period)
Kuruhusu Uhuru wa Vyama vya Siasa, Vyombo vya Habari
Nidhamu makazini( ameagiza wasiinue mabega)
Kuthamini Utu (Mahakama zinahusika hapa)
Uchaguzi Huru na wa Haki
Tume Huru
Katiba mpya (amesema tusubiri kidogo)
Zaidi Kujenga na Kuimarisha Umoja Upendo Aliyotuachia Baba wa Taifa
Si swala la kuvaa au kuvua viatu vya mtu
Rais Mpya ni Mama Samia yeye kama yeye
Yaliyopita si ndwele
Ana mapungufu ni mwanadamu
Akikosea atashauriwa atakosolewa hivyo tu
Yaani hi komenti yako ndio ilifaa kuwa mada yenyewe.Rais Mama Samia Suluhu Hassan hapaswi kuvaa viatu au kutembelea kivuli cha Mwendazake Hayati JPM.
Mzee Ruksa hakutembelea kivuli cha Mwl Nyerere,Marehemu Mzee Mkapa hakutembelea kivuli cha Mzee Ruksa vile vile Mzee wa Msoga hakutembelea kivuli cha Mkapa.
Ikiwa wengi hawakutembelea vivuli vya watangulizi wao kwanini Rais Mama Samia atembelee kivuli cha mwendazake.
Rais Mama Samia kumuhimiza au kumtaka kwa namna yoyote atende kama mtangulizi wake kwa maoni yangu mimi ni kumkosea heshima.Yaani mnataka Mama naye aanze kubambika kesi,atudanganye ATCL inatoa gawio kumbe mihasara kibao,au na yeye ajenge Chake Chake International Airport ndio muone kafanana na Magufuli.Enzi za Magufuli zimepita kama ziluvyopita enzi za Mwl Nyerere.Tuondolee uchuro wa Magufuli utawala wake ulimalizika Rais Mama Samia alipakula kiapo.
Mkuu sio kazi Sana ,ila mama kazi kutokana na Jiwe kuvuruga misingi ya utawala Bora inabidi mama aanze upya.Ila jamani kuwa kiongozi kazii!!!
Najiuliza huyo m'mama sijui m'bibi kama atakuwa na wasaa wa kupita JF akasoma japo headings tu za post zinazotumwa humu wajumbe wakiwa na matumaini makubwa kwenye uongozi wake hakika kesho hataamka maana ni pressure tu.
Safi Sana Mkuu wewe pia umeona wanavyohangaika kutaka kumpush mama afate njia ovu.Team JPM mnapush ajenda zenu kwa kisingizio cha viatu vya Magufuli.. no one is going to buy your propaganda Mr.
HE Samia ameanza vizur sana, tumpe nafasi aoneshe uwezo wake
1.Ubabe kwenye kodi
2.Demokrasia
3.Diplomacy
4.Media freedom
5. Kazi zenye Tija
Hiyo miradi "mikakati" ya wiz simshauri hata kidogo
Maoni Safi Sana haya kuliko hoja za mtoa mada.Akifuata katiba,hakuna kitu kigumu. Hakuna cha kiatu cha magufuli au kivuli cha magufuli. Hapa ni maisha yanaendelea kama kawaida tu. Alikuwa ni wa kawaida kama wanadamu wengine tu. Aliyoyafanya aliyoyafanya kwa sababu ni mwajiriwa kama wengine waliokuwa wakilipwa na fedha za umma. Kwa hiyo,tumwache huyu aliyeingia naye afanye kwa mujibu wa katiba na asijaribu kufanya nje ya maamuzi sahihi kwa mujibu wa katiba na sheria zinazomwongoza.
Majukumu tofauti kwa hao watu ni kama yapi?...taja mfano ikibidi...namshauri Raisi Samia Hassan awapangie majukumu tofauti wahusika wa genge la watu WASIOJULIKANA.
..Tanzania bila matusi, ubaguzi, na ukatili, inawezekana.
Majukumu tofauti kwa hao watu ni kama yapi?...taja mfano ikibidi.
...vipi kuhusu waliohujumiwa na hao jamaa, wao watapataje haki yao?...hili genge kulishitaki inaweza kuwa ni kazi ngumu.
..kwa hiyo wapangiwe majukumu mengine yatayawapatia kipato halali.
Sawa mkuu. Pole sana kwa msiba. Nakwambia kwa dhati kabisa kwa sababu japo msiba ni wote sote. Wewe umekugusa kwa namna ya pekee.Kinyungu, Kinyungu. Naomba ujue ya kwamba, mapenzi yangu kwa JPM are "untainted".
Ni kweli. Hebu chukua mfano wa rais kujibu maswali ya waandishi wa habari na wananchi kwa ujumla. Mimi nilishasahau kama rais anatakiwa kuulizwa maswali na kutoa majibu mara kwa mara. Mwendazake alishafanya nchi kama ufalme wake, hakuna kuuliza hakuna kuhoji. Hili rais Samia anatakiwa alifutilie mbali na awe anafanya mikutano na waandishi mara kwa mara kujibu na kufafanua mambo ya kitaifa na kimataifa.Uongozi wa Magufuli ulikuwa wa propaganda na uonevu mkubwa, siyo aina ya utawala wa kuchukulia mfano mwema.
ni disaster haufai!
Kamtaja Magufuli mara 200🤣🤣🤣🤣🤣Makala ndefu saaaanaaa. Huo muda wa kuandika unautoa wapi?
Nakubaliana na wewe 100%.Rais Mama Samia Suluhu Hassan hapaswi kuvaa viatu au kutembelea kivuli cha Mwendazake Hayati JPM.
Mzee Ruksa hakutembelea kivuli cha Mwl Nyerere,Marehemu Mzee Mkapa hakutembelea kivuli cha Mzee Ruksa vile vile Mzee wa Msoga hakutembelea kivuli cha Mkapa.
Ikiwa wengi hawakutembelea vivuli vya watangulizi wao kwanini Rais Mama Samia atembelee kivuli cha mwendazake.
Rais Mama Samia kumuhimiza au kumtaka kwa namna yoyote atende kama mtangulizi wake kwa maoni yangu mimi ni kumkosea heshima.Yaani mnataka Mama naye aanze kubambika kesi,atudanganye ATCL inatoa gawio kumbe mihasara kibao,au na yeye ajenge Chake Chake International Airport ndio muone kafanana na Magufuli.Enzi za Magufuli zimepita kama ziluvyopita enzi za Mwl Nyerere.Tuondolee uchuro wa Magufuli utawala wake ulimalizika Rais Mama Samia alipakula kiapo.