Vibaka wamerudi mtaani kwa wingi

Vibaka wamerudi mtaani kwa wingi

Naomba Jeshi la Polisi hasa mitaani mje kusaidia maana vibaka wamerudi kwa wingi sana. Hii sio siasa ni reality kabisa na siandiki kwa mihemuko!

Kuna kipindi tulianza kulala milango wazi lakini kwa sasa wanakata mpaka madirisha

Kwanini utake kulala mlango wazi, wacha ushtuliwe ili akili ikukae sawa, ww unataka ulale kama mfu, eti mlango wazi, lazima ujue kulinda nyumba yako na mali zako, kuanzia nyumbani hadi accounts zako, don't trust anyone likija suala la security yako, na usitegemee polisi kwa 100%, ww binafsi ndio mlinzi namba moja wa mali zako.

Weka mazingira magumu kwa mwizi kukuingilia, madirisha weka nondo, mageti milango nondo sio flat bars, kama ni ukuta wa geti uwe mrefu na juu weka security cameras kama una uwezo.

Sasa ww unataka kulala milango wazi? Be serious plz, acha utoto
 
Vibaka hawajawi kuisha hata kipindi cha mwendazake, ila sasa hivi vyombo vya habari viko huru kutangaza huo uhuni. Ulifumbwa macho na propaganda mfu ndio maana unaleta huu uzi kwa rejea za utawala wa mabavu.
Kwahyo unataka kusema kisa JPM alikuwepo ,vyombo vya habari viliogopa mpka kutangaza wezi?

Hujitambui kbsa mkuu

Sent from my Infinix X683 using JamiiForums mobile app
 
Huwa najiuliza hawa vibaka umri ukisonga huwa wanakwendaga wapi ? au wao huwa wako hivyo hivyo miaka yote.
 
Weka ushahidi. Usichafue jeshi la Sirro kuwa limeshindwa kazi.
Manispaa ya Ilemela wana gari la doria moja tu, polisi wanalitumia kutafutia hela ya dawa ya viatu usiku...watu wanakabwa, nyumba zinavamiwa ukiwapigia simu polisi wanasema wapo Kayenze (nje ya mji hukoo) kumbe wapo wanavizia sehemu zenye ulaji!!!

Ukweli huchelewa kufika ila uongo huwa unawahi, ngojeni muone kama hatujarudi kule kule enzi za hakimu kushindwa kutoa hukumu kisa hakuna karatasi za kuandikia.
Acha niendelee kuishi kijijini maana hali ya mjini kwa sasa ni hatari tupu!
 
Huwa najiuliza hawa vibaka umri ukisonga huwa wanakwendaga wapi ? au wao huwa wako hivyo hivyo miaka yote.
Wanakuwa wanasiasa mfano yule mbuge mstaafu wa Arusha ambaye yupo uhamishoni, wengine huwa wachungaji, nk
 
Naomba waendelee kuwepo na wakabe sana mpaka rais wakamkabe hakuna jinsi
Pic%20Layer_202111923101073.jpg
 
Vibaka hawajawahi kupungua wakati wowote na ndio maana siku zote tunahamasishwa kuwa na ulinzi shirikishi.
 
Zanzibar kibaka akikamatwa na kuthibitika kama ametenda wizi basi wanamkata mkono,watu wenye hasira kali siku hizi wamezidi sana pale Zanzibar hawana masihara wanakumega mkono kisha wanakwambie tembea au potea..
 
Mabasi yanatekwa
Albino wanauawa tena
Mauaji ya wakulima na wafugaji
Yamerudi kwa kasi ya radi.
 
Mwendazake amekujaje kwenye hii mada
Vibaka hawajawi kuisha hata kipindi cha mwendazake, ila sasa hivi vyombo vya habari viko huru kutangaza huo uhuni. Ulifumbwa macho na propaganda mfu ndio maana unaleta huu uzi kwa rejea za utawala wa mabavu.
 
Mkiwanasa wakateni mkono au huko hakuna watu wenye hasira kali ,ile serikali ile ilikuwa na watu wasiojulikana wananchi ni lazima nanyi muwe na watu wenye hasira kali ,tuone vibaka watatafuta mitaa ya kwenda kufanya uhuni wao, Muroko wa dodoma akiwaambia Dodoma sio sehemu ya kuendesha uhuni wao wakatafute mikoa mingine. Sasa Dodoma ni shwari kabisa tunalala milango wazi na vyoo tunaweka milango ya matambara tu.
 
Back
Top Bottom