astalavista
Senior Member
- Jul 7, 2014
- 156
- 160
Nimeona na baadhi ya maeneo uwekaji wa vibao vya barabara na mitaa namna ambavyo imeacha maswali kwa wananchi, binafsi nimeyakuta haya Masasi hasa vijiji vya Masasi Dc.
Wakati zoezi linaanza nilifikiri pengine utaratibu mpya wa kupata majina na vibao elekezi vya mitaa na barabara lingefanyika kwa weledi na umakini wa hali juu ili kuwa mpango utakaodumu muda mrefu.
Ajabu yapo maeneo vibao vimewekwa kwenye Miembe, Mikorosho, kadhalika yapo maeneo ambayo nguzo zilizobeba vibao ni miti ya mwarobaini na Msonobari, miti ambayo haiwezi kuwa imara kwa muda mrefu.
Rai yangu kwa Mamlaka husika, nikimlenga zaidi waziri mwenye dhamana kaka yangu Nape Nnauye kulitazama hili kwa ukaribu zaidi, jambo ni zuri lakini kinachoendelea sasa kwa watendaji huku chini ni kuichafua dhamira ya serikali.