Vibarua kiwanda cha Bakhresa Buguruni

Evah manpower supply [emoji1][emoji1][emoji1][emoji1] Dahh fursa ni nyingi sana humu duniani.
 
Mkuu najua ugumu na maumivu ya kuishi bila kazi hasa hapa mjini. Aisee pale kazi zipo huwezi kwenda pale ukakosa kazi lakini ndugu yangu UNA MANGUVU? Mkuu pale kuna ule mpigiko ambao utahisi dunia imekuacha, ni rahisi watu kusema ni bora hicho kidogo kuliko kukosa kabisa lakini nakuhakikishia kuwa aslimia zaidi ya 50 ya vibaruq pqle huacha kazi siku ya kwanza halafu aslimia 30 huvumilia hadi mwisho wa wiki.

Yupo jamaa yangu anaitwa Ngosha ni wale wasukuma wazee wa kazi nzito, aisee mbona aliingia pale akatema mzigo siku ya kwanza. We fikiria kupiga kazi ngumu haswa kwa masaa 12 halafu unarudi nyumbani na 2000 hapo hatujapigia nauli.
Na ubaya zaidi wa ile kazi haupati nafasi ya kusema unaweza kutoka pale ukapata muda wa kwenda kuzurula kutafuta vibarua sehemu nyingine.
Yamkini bahati ipo kwako na una huo moyo na uwezo wa mapambano nenda kajaribu bahati yako. Lakini kwa umbali wa Bunju sioni kama itakua na manufaa sana kwako maana hata nauli ya kurudi unaweza kukosa.

Iwapo unatokea Bunju nauli pekee kwa siku ni karibu 3000, ukiwa pale kiwandani tudanye umepiga chai ya buku na lunch ya 1500. Ukanywa maji ya jero. Halafu mwisho wa siku ukalipwa 4000 aisee itakua ni balaa. Piga hesabu zako vizuri mkuu na ninakuombea kheri kwa Mungu akusaidie katika mapambano haya.
 
Jamani naomba msaada wa kupata kazi mambo magumu vibaya mno.
Jinsia ni mwanaume
Umri miaka 25
Elimu kidato cha sita
Naishi D'Salaam
Natanguliza shukrani[emoji1488]
Kijana mwenzagu. Maisha hayasubiriwi.. Yatafute ili watu was iwe wabaya. Anza hata na uwinga kariakoo Kuna digrii nyingi sana mule zinadanda danda
 
Umenikumbusha kuna siku nilienda omba ruhusa kwa mchina maana nilikua naumwa sasa kipara akawa anatafsiri tofauti nikashangaa mchina anawaka nikaanza pigwa mateke sa sikujua alimwambia nini
Labda alimwambia hivi mchina " huyu anasema wewe ni msengΒ£ na huna lolote mvimba macho mmoja wewe"
Mchina akaanza kukubutua mateke.
🀣🀣🀣🀣🀣🀣🀣
Halafu nasikia kuna viwanda vya wachina huko Kongowe na pwani ,kuna wachina wanatandika vibarua na wafanyakazi bakora kabisa ,mamaye navunja mtu koromeo ,utakuta kuna zoba linaambiwa lala chini ,lina tandikwa mboko na linakubali 🀣🀣🀣🀣,ukisikia modern slavery ndio hii ,a slave without shackles
 
Si bora hiyo kuliko kukaa idle ukihesabu nyota angani
Hili utalisema kama hujafanya hiyo kazi. Lakini siku ukienda na kupigiga sawa sawasawa utasema bora kwenda kushika jemba kuliko kuteseka namna hiyo. Halafu kazi kama hizi zinakuathiri kiafya. Umri ukienda kidogo unaweza kujikuta magonjwa hayaishi kukuandama.
 
Daah! Pole sana aisee mkuu.
 
"...criminal cartels za mamafia..."
[emoji115][emoji115]
Hahahahahaha criminal cartels za nani[emoji38][emoji38][emoji38][emoji38][emoji38][emoji38]
 
Mkiwa na raia wengi sana ndan ya nchi at the end of the day mnageuka kuwa cheap labours

Just imagine ndan ya miaka 10 tu wamezaliwa na kuongezeka raia zaidi 16ml
Control population you control the economy
Kwahio hawa waliozaliwa ndani ya miaka 10 tayari wanaingia kwenye soko la ajira sio
 
Hiyo kazi ya heshima kabisa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…