Vibarua kiwanda cha Bakhresa Buguruni

Vibarua kiwanda cha Bakhresa Buguruni

Archana na bakhresa,huku pwani kuna kiwanda cha sabuni kinaitwa ked's kinazalishasabuni za doffi na kleesoft vibarua wanalipwa na wakala aliyeingia ubia na kampuni hii ....sasa utakuta wakala analipwa sh 12,000 kwa Kila kibarua Ila yeye analipa sh 8000 kwa Kila kibarua ...
Wanateswa Sana vijana...huyo wakala anaitwa EVAH MANPOWER SUPPLIES..kiongozi wao anaitwa kipara...
Evah manpower supply [emoji1][emoji1][emoji1][emoji1] Dahh fursa ni nyingi sana humu duniani.
 
Mkuu najua ugumu na maumivu ya kuishi bila kazi hasa hapa mjini. Aisee pale kazi zipo huwezi kwenda pale ukakosa kazi lakini ndugu yangu UNA MANGUVU? Mkuu pale kuna ule mpigiko ambao utahisi dunia imekuacha, ni rahisi watu kusema ni bora hicho kidogo kuliko kukosa kabisa lakini nakuhakikishia kuwa aslimia zaidi ya 50 ya vibaruq pqle huacha kazi siku ya kwanza halafu aslimia 30 huvumilia hadi mwisho wa wiki.

Yupo jamaa yangu anaitwa Ngosha ni wale wasukuma wazee wa kazi nzito, aisee mbona aliingia pale akatema mzigo siku ya kwanza. We fikiria kupiga kazi ngumu haswa kwa masaa 12 halafu unarudi nyumbani na 2000 hapo hatujapigia nauli.
Na ubaya zaidi wa ile kazi haupati nafasi ya kusema unaweza kutoka pale ukapata muda wa kwenda kuzurula kutafuta vibarua sehemu nyingine.
Yamkini bahati ipo kwako na una huo moyo na uwezo wa mapambano nenda kajaribu bahati yako. Lakini kwa umbali wa Bunju sioni kama itakua na manufaa sana kwako maana hata nauli ya kurudi unaweza kukosa.

Iwapo unatokea Bunju nauli pekee kwa siku ni karibu 3000, ukiwa pale kiwandani tudanye umepiga chai ya buku na lunch ya 1500. Ukanywa maji ya jero. Halafu mwisho wa siku ukalipwa 4000 aisee itakua ni balaa. Piga hesabu zako vizuri mkuu na ninakuombea kheri kwa Mungu akusaidie katika mapambano haya.
 
Jamani naomba msaada wa kupata kazi mambo magumu vibaya mno.
Jinsia ni mwanaume
Umri miaka 25
Elimu kidato cha sita
Naishi D'Salaam
Natanguliza shukrani[emoji1488]
Kijana mwenzagu. Maisha hayasubiriwi.. Yatafute ili watu was iwe wabaya. Anza hata na uwinga kariakoo Kuna digrii nyingi sana mule zinadanda danda
 
Umenikumbusha kuna siku nilienda omba ruhusa kwa mchina maana nilikua naumwa sasa kipara akawa anatafsiri tofauti nikashangaa mchina anawaka nikaanza pigwa mateke sa sikujua alimwambia nini
Labda alimwambia hivi mchina " huyu anasema wewe ni mseng£ na huna lolote mvimba macho mmoja wewe"
Mchina akaanza kukubutua mateke.
🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣
Halafu nasikia kuna viwanda vya wachina huko Kongowe na pwani ,kuna wachina wanatandika vibarua na wafanyakazi bakora kabisa ,mamaye navunja mtu koromeo ,utakuta kuna zoba linaambiwa lala chini ,lina tandikwa mboko na linakubali 🤣🤣🤣🤣,ukisikia modern slavery ndio hii ,a slave without shackles
 
Si bora hiyo kuliko kukaa idle ukihesabu nyota angani
Hili utalisema kama hujafanya hiyo kazi. Lakini siku ukienda na kupigiga sawa sawasawa utasema bora kwenda kushika jemba kuliko kuteseka namna hiyo. Halafu kazi kama hizi zinakuathiri kiafya. Umri ukienda kidogo unaweza kujikuta magonjwa hayaishi kukuandama.
 
SITOSAHAU SIKU NILIPOTAKA KUFA PALE KIWANDANI

Ilikua mapema mwaka jana nilipitia kipindi kigumu sana baada ya kuyumba kiuchumi na degree yangu mkononi ikanilazimu kujizima data na kutafuta kazi yoyote iwe rasmi au isiwe rasmi.Nikazama zangu jf ndipo nikapata muongozo wa kwenda kiwanda cha unga kwa kurubuniwa kwamba kwa siku malipo inafika hadi buku 8 nikajipa. moyo..

Basi nikafata tafatibu zote siku ya pili nikaenda na barua ya mtendaji then nikaambiwa siku ya pili usiku nikaanze kazi.Basi bwana nikazama zangu pale mida ya saa 1 jioni nikawakuta wenzangu wapo tayari wanasubiri kuanza kazi.Wakagawa msosi pale ndani kila mtu sahani ya wali(upo kama makande) na maharage na ndizi mbivu.Kwa kua ni siku ya kwanza nikawa na uoga uoga wa kula ule msosi na niliogopa kuja kukatwa kwenye malipo[emoji28].Jamaa wakawa wananishangaa huyu msela vipi huu msosi ni lazima kuchukua haijalishi unataka au hutaki.Basi kuna jamaa akasema chukua nipe mm nitakula,wakawa wanagombania nipe mim nipe mimi.Basi nikachukua ule msosi nikampa jamaa mmoja akala na wa kwake.

Kimbembe kilianza baada ya masaa mawili viroba vilipoanza kushika toka kwenye vinu vinashuka kama mvua na vinu vipo vya kutosha mule ndani.Ili kusubiria viwe vingi ndio kazi ianze wale jamaa wakasema tuchezeni boli humu ndani(mpira wa makaratasi).Basi tukagawana huku na huku tukaanza kucheza mpira.Katika harakati za kuucheza ule mpira nikajibamiza vibaya sana kwenye kinu kipo kama upinde afu kule mbele kama wembe kwa makali yake.Ghafla bin vuu nikajikuta nipo chini nimezungukwa na watu kibao damu zinavuja kama kuku katoka kuchinjwa..Aisee nilijua leo ndio siku yangu siwezi kutoboa maana nilipasuka katikati ya kichwa.Wakaniinua pale sina hata nguvu wakasema nikapumzike pale kazi inataka kuanza.Nilishindwa coz damu zilikua zinavuja sana kuna jamaa akanielekezaa bafu akasema nikaoge ili niwe sawa.

Nilijivuta nikaenda kuoga kule bafuni maji yote yalijaa damu tu yani ili siku ilikua ndio bye bye sema Mungu hakupanga tu.Nikarudi kule ndani jamaa ndio wanagawana watu kwa makundi waanze kazi.Cha ajabu na mimi nikaitwa nikapangiwa kundi nibebe viroba.Nikawaeleza siko sawa damu zinavuja sana lakini hakuna aliyeelewa.Wakasema humu ndani ni lazima kila mtu afanye kazi.Kazi ikaanza nikaambiwa na mm nibebe kichwani zile kilo 25 kwa 50 yena viwili trip moja.Ilikua ngumu sana kubeba lakini sikua na jinsi nikajaribu tripu moja nakashindwa kichwa kilikua kinauma sana.Wakanibadilisha section wakasema niwe nawapakia watu kichwani wenyewe wanaita kijiko,yani unabeba viroba viwili pale chini na kumpa mtu kichwani.Nimefanya mara moja tu kuna jamaa akanigusa pale kichwani na kiroba basi damu zikaanza upya kutoka nikaamua kuacha nikasema liwalo na liwe cha kufia nini.

Basi nikatoka pale nikaenda nje kukaa toka ile saa 4 mpaka saa 12 asubuhi jamaa wanabeba tu vile viroba.Walikua kama 30 hivi lakini viroba walivyobeba ni zaidi ya 6,000 yani kila mmoja kama mia 2 hivi.Asubuhi ya saa 1 tukaitwa wote kwenye mgao wa pesa.Kaja kiongozi wao akasema leo kazi hamna hivyo kila mtu atapata elfu 2,aisee nilichoka mwili na akili yani kazi yote ile mtu alipwe elfu 2.Kuna watu walikua wanapinga mm kupewa ile elfu 2 kisa sijafanya kazi.Sema jamaa akanipa ile buku 2 akasema ukatibiwe.Nimetoka pale naona kama ndoto nikarudi zangu geto ile pesa nikafanya nauli sikubakiwa hata na senti..

Nimefika home kichwa chote kimeloa damu na nimepasuka vibaya sana.Sikua na pesa hivyo nikachukua chumvi na beseni nikaanza kujisafisha huku nikipata maumivu makali sana.Sikwenda kabisa hospitali hadi leo hii na nilipona kwa uwezo wa Mungu baada ya mwezi kupita.Nashukuru hivi sasa nipo sehemu nzuri japo sio sana ila sio kama mwanzo.Leo nilipita ile njia ya kiwandani nikakumbuka kuleta kisa hiki.
View attachment 2484012
Daah! Pole sana aisee mkuu.
 
Kazi za viwandani hasa Tanzania ni hatari sana kwa afya na uhai wako ,do it for your own risk , safety zero ,vitendea kazi hamna ,mazingira mabovu na hatarishi kwa afya na uhai , ujira mdogo sana na usiofaa kabisa + manyanyaso na overwork .
Compliance ya OSHA (Occupation safety and health ) ni always zero ,hivyo ndio viwanda uchwara vya bongo.
Kuna mdau kaongelea kiwanda cha NONDO Nyakato steel-Mwanza , kile ni mfano mmoja wapo , mwaka jana hapo Nyakato steel bomu lilipuka humo ndani ,yote hiyo ni uzembe wa compliance ya masuala ya safety ,wao wanafanya biashara ya kuteyusha chuma chakavu yet hamna mifumo thabiti ya kuchunguza na kusort vyuma vinavyoletwa ili kuyeyushwa ,matokeo yake wanaokoteza kila aina ya chuma na kuvipeleka kwenye vinu /furnaces kuyeyushwa ,upuuz mtupu .
Hivi viwanda vingi bongo vinaoperate kama criminal cartels za mamafia ,Kwanza wengi wanaoendesha hivyo viwanda ni matapeli tu ,wanatapeli hata hivyo viposho vya elfu mbili mbili wanavyowalipa hao vibarua utakuta kuna muda hawawalipi ,mambo ya ovyo kabisa
"...criminal cartels za mamafia..."
[emoji115][emoji115]
Hahahahahaha criminal cartels za nani[emoji38][emoji38][emoji38][emoji38][emoji38][emoji38]
 
Mkiwa na raia wengi sana ndan ya nchi at the end of the day mnageuka kuwa cheap labours

Just imagine ndan ya miaka 10 tu wamezaliwa na kuongezeka raia zaidi 16ml
Control population you control the economy
Kwahio hawa waliozaliwa ndani ya miaka 10 tayari wanaingia kwenye soko la ajira sio
 
Itoshe kusema tu kwamba kupitia huu uzi nimejifunza kwamba nisiidharau kazi yangu ya Bodaboda maana nina degree yangu hapa inanifanya niidharau hii kazi ya Boda naona kama sistahili kuifanya kumbe kuna watu wanapigika kinoma tena kwa malipo madogo sana kwa siku nzima wakati mie kwenye boda naweza pata mara Tano ya wao [emoji119]

Maisha yamenifundisha kuwa ukitaka kuijua thamani ya neema yoyote uliyojaaliwa na M/Mungu basi jilinganishe na walio chini yako usijilinganishe na walio juu yako.
Hiyo kazi ya heshima kabisa
 
Back
Top Bottom