Vibarua kiwanda cha Bakhresa Buguruni

Vibarua kiwanda cha Bakhresa Buguruni

SITOSAHAU SIKU NILIPOTAKA KUFA PALE KIWANDANI

Ilikua mapema mwaka jana nilipitia kipindi kigumu sana baada ya kuyumba kiuchumi na degree yangu mkononi ikanilazimu kujizima data na kutafuta kazi yoyote iwe rasmi au isiwe rasmi.Nikazama zangu jf ndipo nikapata muongozo wa kwenda kiwanda cha unga kwa kurubuniwa kwamba kwa siku malipo inafika hadi buku 8 nikajipa. moyo..

Basi nikafata tafatibu zote siku ya pili nikaenda na barua ya mtendaji then nikaambiwa siku ya pili usiku nikaanze kazi.Basi bwana nikazama zangu pale mida ya saa 1 jioni nikawakuta wenzangu wapo tayari wanasubiri kuanza kazi.Wakagawa msosi pale ndani kila mtu sahani ya wali(upo kama makande) na maharage na ndizi mbivu.Kwa kua ni siku ya kwanza nikawa na uoga uoga wa kula ule msosi na niliogopa kuja kukatwa kwenye malipo[emoji28].Jamaa wakawa wananishangaa huyu msela vipi huu msosi ni lazima kuchukua haijalishi unataka au hutaki.Basi kuna jamaa akasema chukua nipe mm nitakula,wakawa wanagombania nipe mim nipe mimi.Basi nikachukua ule msosi nikampa jamaa mmoja akala na wa kwake.

Kimbembe kilianza baada ya masaa mawili viroba vilipoanza kushika toka kwenye vinu vinashuka kama mvua na vinu vipo vya kutosha mule ndani.Ili kusubiria viwe vingi ndio kazi ianze wale jamaa wakasema tuchezeni boli humu ndani(mpira wa makaratasi).Basi tukagawana huku na huku tukaanza kucheza mpira.Katika harakati za kuucheza ule mpira nikajibamiza vibaya sana kwenye kinu kipo kama upinde afu kule mbele kama wembe kwa makali yake.Ghafla bin vuu nikajikuta nipo chini nimezungukwa na watu kibao damu zinavuja kama kuku katoka kuchinjwa..Aisee nilijua leo ndio siku yangu siwezi kutoboa maana nilipasuka katikati ya kichwa.Wakaniinua pale sina hata nguvu wakasema nikapumzike pale kazi inataka kuanza.Nilishindwa coz damu zilikua zinavuja sana kuna jamaa akanielekezaa bafu akasema nikaoge ili niwe sawa.

Nilijivuta nikaenda kuoga kule bafuni maji yote yalijaa damu tu yani ili siku ilikua ndio bye bye sema Mungu hakupanga tu.Nikarudi kule ndani jamaa ndio wanagawana watu kwa makundi waanze kazi.Cha ajabu na mimi nikaitwa nikapangiwa kundi nibebe viroba.Nikawaeleza siko sawa damu zinavuja sana lakini hakuna aliyeelewa.Wakasema humu ndani ni lazima kila mtu afanye kazi.Kazi ikaanza nikaambiwa na mm nibebe kichwani zile kilo 25 kwa 50 yena viwili trip moja.Ilikua ngumu sana kubeba lakini sikua na jinsi nikajaribu tripu moja nakashindwa kichwa kilikua kinauma sana.Wakanibadilisha section wakasema niwe nawapakia watu kichwani wenyewe wanaita kijiko,yani unabeba viroba viwili pale chini na kumpa mtu kichwani.Nimefanya mara moja tu kuna jamaa akanigusa pale kichwani na kiroba basi damu zikaanza upya kutoka nikaamua kuacha nikasema liwalo na liwe cha kufia nini.

Basi nikatoka pale nikaenda nje kukaa toka ile saa 4 mpaka saa 12 asubuhi jamaa wanabeba tu vile viroba.Walikua kama 30 hivi lakini viroba walivyobeba ni zaidi ya 6,000 yani kila mmoja kama mia 2 hivi.Asubuhi ya saa 1 tukaitwa wote kwenye mgao wa pesa.Kaja kiongozi wao akasema leo kazi hamna hivyo kila mtu atapata elfu 2,aisee nilichoka mwili na akili yani kazi yote ile mtu alipwe elfu 2.Kuna watu walikua wanapinga mm kupewa ile elfu 2 kisa sijafanya kazi.Sema jamaa akanipa ile buku 2 akasema ukatibiwe.Nimetoka pale naona kama ndoto nikarudi zangu geto ile pesa nikafanya nauli sikubakiwa hata na senti..

Nimefika home kichwa chote kimeloa damu na nimepasuka vibaya sana.Sikua na pesa hivyo nikachukua chumvi na beseni nikaanza kujisafisha huku nikipata maumivu makali sana.Sikwenda kabisa hospitali hadi leo hii na nilipona kwa uwezo wa Mungu baada ya mwezi kupita.Nashukuru hivi sasa nipo sehemu nzuri japo sio sana ila sio kama mwanzo.Leo nilipita ile njia ya kiwandani nikakumbuka kuleta kisa hiki.
View attachment 2484012

Duh kwel kuna watu wanapitia magum sana
 
Jamaa yangu mmoja aliambiwa atoe 50k apate kazi mpaka leo hajapata ameamua kusamehe. Kuna rushwa sana Keds na ukiritimba wa hali ya juu.
2017 nilihangaika sana kuomba kazi pale lakini wapi mpaka nikakata tamaa!
Poole mkuu.
Mi nilishawahi pata kazi pale na ilikua bahati tu maana nilipewa namba ya hr na watu tulokua tunakaa pale nje kusubiri vibarua nikampigia akanambia tu njoo kesho asubuhi .

Nilienda nikafanya interview pale akacheki vyeti vyangu akanipeleka kwa mchina kule Nako nikaulizwa maswali machache nikajibu then nikapewa form ya hospital nikajaze na niliporudisha form ndo nikaanza kazi.

Sikuwahi kupewa mkataba na nilikua nalipwa kama kibarua tu na kipindi hicho wanalipwa 10000 per day.
 
Poole mkuu.
Mi nilishawahi pata kazi pale na ilikua bahati tu maana nilipewa namba ya hr na watu tulokua tunakaa pale nje kusubiri vibarua nikampigia akanambia tu njoo kesho asubuhi .

Nilienda nikafanya interview pale akacheki vyeti vyangu akanipeleka kwa mchina kule Nako nikaulizwa maswali machache nikajibu then nikapewa form ya hospital nikajaze na niliporudisha form ndo nikaanza kazi.

Sikuwahi kupewa mkataba na nilikua nalipwa kama kibarua tu na kipindi hicho wanalipwa 10000 per day.
Siku hizi wamepunguza kiwango cha malipo nadhani ni 7500 au 8000.
Mimi bwana nilipata nafasi ya kuingia hadi kule ndani nikakutanishwa na jamaa mmoja hivi, kanichimba chimba biti pale dogo unaweza kazi nikamjibu naweza njoo uone kazi nikapelekwa kwa washkaji wanachimba mashimo sijui yalikuwa ya choo yale aseee jamaa akaniuliza unaweza kazi nikajitutumua naweza bro, akaniambia basi nipe namba yako na majina yako nitakuita, aah wapi nikajua hapa nishalambwa kichwa!!
 
Siku hizi wamepunguza kiwango cha malipo nadhani ni 7500 au 8000.
Mimi bwana nilipata nafasi ya kuingia hadi kule ndani nikakutanishwa na jamaa mmoja hivi, kanichimba chimba biti pale dogo unaweza kazi nikamjibu naweza njoo uone kazi nikapelekwa kwa washkaji wanachimba mashimo sijui yalikuwa ya choo yale aseee jamaa akaniuliza unaweza kazi nikajitutumua naweza bro, akaniambia basi nipe namba yako na majina yako nitakuita, aah wapi nikajua hapa nishalambwa kichwa!!
Pale mkuu wajanja wengi sana unaweza pigwa hela na kazi usipate.
 
Nakumbuka nilishawahi fanya kazi kiwanda cha kusaga chai yaani unaingia asubuhi saa 12 unatoka jioni saa 12 au saa zingine unatoka asubuhi kesho yake kwa ujira wa 2500/day na hakuna overtime.... Maisha ni safari mazee.
 
Wanalipa elfu nne hadi tatu then Kazi ni kubeba viroba vya ngano kilo 50 na 25 Kuanzia asubuhi Hadi jioni na pia night shift hipo it about fucking job huyo Bakhressa Ni mpuuzi mmoja. Including Mo dewij and so called matajiri uchwara
Wao hawana shida, shida ni Serikali ya CCM imewapagia kiwango cha kulipa vibarua, Zanzibar wao vibarua analipwa elf 15 serikali ya Dr Shein ilipaga hivyo, Na uku Serikali ikisema kibarua alipwe elfu 10 wahindi watalipa tu wao wanasema wafata Bei elekezi ya serikali
 
Kuna jamaa yangu aliona makaratasi ya ajira viwandani wamebandika katika nguzo za umeme mshahara kwa wiki ni laki 275,000/= .jamaa akajitosa akawahi asubuhi saa 12 yupo getini kufika mida ya saa 5 asubuhi namuona jamaa huyu hapa gheto namuuliza mbona umewahi kurudi mapema yote hii kulikoni?
Jamaa akaniambia brother acha tu uliona wapi watu wawili mmekabidhiwa Lori scania 10 zimejaa mzigo wa gypsum board muushushe mzigo wote kwa siku moja?[emoji2]
Jamaa alipiga kazi mpaka saa 5 asubuhi alivyoona hakuna dalili ya mzigo kuisha akaamua kutoroka.
Hapo hata mimi lazima tu nile kona [emoji1732][emoji23]

Sent from my CPH2387 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom