Vibarua kiwanda cha Bakhresa Buguruni

Vibarua kiwanda cha Bakhresa Buguruni

SITOSAHAU SIKU NILIPOTAKA KUFA PALE KIWANDANI

Ilikua mapema mwaka jana nilipitia kipindi kigumu sana baada ya kuyumba kiuchumi na degree yangu mkononi ikanilazimu kujizima data na kutafuta kazi yoyote iwe rasmi au isiwe rasmi.Nikazama zangu jf ndipo nikapata muongozo wa kwenda kiwanda cha unga kwa kurubuniwa kwamba kwa siku malipo inafika hadi buku 8 nikajipa. moyo..

Basi nikafata tafatibu zote siku ya pili nikaenda na barua ya mtendaji then nikaambiwa siku ya pili usiku nikaanze kazi.Basi bwana nikazama zangu pale mida ya saa 1 jioni nikawakuta wenzangu wapo tayari wanasubiri kuanza kazi.Wakagawa msosi pale ndani kila mtu sahani ya wali(upo kama makande) na maharage na ndizi mbivu.Kwa kua ni siku ya kwanza nikawa na uoga uoga wa kula ule msosi na niliogopa kuja kukatwa kwenye malipo[emoji28].Jamaa wakawa wananishangaa huyu msela vipi huu msosi ni lazima kuchukua haijalishi unataka au hutaki.Basi kuna jamaa akasema chukua nipe mm nitakula,wakawa wanagombania nipe mim nipe mimi.Basi nikachukua ule msosi nikampa jamaa mmoja akala na wa kwake.

Kimbembe kilianza baada ya masaa mawili viroba vilipoanza kushika toka kwenye vinu vinashuka kama mvua na vinu vipo vya kutosha mule ndani.Ili kusubiria viwe vingi ndio kazi ianze wale jamaa wakasema tuchezeni boli humu ndani(mpira wa makaratasi).Basi tukagawana huku na huku tukaanza kucheza mpira.Katika harakati za kuucheza ule mpira nikajibamiza vibaya sana kwenye kinu kipo kama upinde afu kule mbele kama wembe kwa makali yake.Ghafla bin vuu nikajikuta nipo chini nimezungukwa na watu kibao damu zinavuja kama kuku katoka kuchinjwa..Aisee nilijua leo ndio siku yangu siwezi kutoboa maana nilipasuka katikati ya kichwa.Wakaniinua pale sina hata nguvu wakasema nikapumzike pale kazi inataka kuanza.Nilishindwa coz damu zilikua zinavuja sana kuna jamaa akanielekezaa bafu akasema nikaoge ili niwe sawa.

Nilijivuta nikaenda kuoga kule bafuni maji yote yalijaa damu tu yani ili siku ilikua ndio bye bye sema Mungu hakupanga tu.Nikarudi kule ndani jamaa ndio wanagawana watu kwa makundi waanze kazi.Cha ajabu na mimi nikaitwa nikapangiwa kundi nibebe viroba.Nikawaeleza siko sawa damu zinavuja sana lakini hakuna aliyeelewa.Wakasema humu ndani ni lazima kila mtu afanye kazi.Kazi ikaanza nikaambiwa na mm nibebe kichwani zile kilo 25 kwa 50 yena viwili trip moja.Ilikua ngumu sana kubeba lakini sikua na jinsi nikajaribu tripu moja nakashindwa kichwa kilikua kinauma sana.Wakanibadilisha section wakasema niwe nawapakia watu kichwani wenyewe wanaita kijiko,yani unabeba viroba viwili pale chini na kumpa mtu kichwani.Nimefanya mara moja tu kuna jamaa akanigusa pale kichwani na kiroba basi damu zikaanza upya kutoka nikaamua kuacha nikasema liwalo na liwe cha kufia nini.

Basi nikatoka pale nikaenda nje kukaa toka ile saa 4 mpaka saa 12 asubuhi jamaa wanabeba tu vile viroba.Walikua kama 30 hivi lakini viroba walivyobeba ni zaidi ya 6,000 yani kila mmoja kama mia 2 hivi.Asubuhi ya saa 1 tukaitwa wote kwenye mgao wa pesa.Kaja kiongozi wao akasema leo kazi hamna hivyo kila mtu atapata elfu 2,aisee nilichoka mwili na akili yani kazi yote ile mtu alipwe elfu 2.Kuna watu walikua wanapinga mm kupewa ile elfu 2 kisa sijafanya kazi.Sema jamaa akanipa ile buku 2 akasema ukatibiwe.Nimetoka pale naona kama ndoto nikarudi zangu geto ile pesa nikafanya nauli sikubakiwa hata na senti..

Nimefika home kichwa chote kimeloa damu na nimepasuka vibaya sana.Sikua na pesa hivyo nikachukua chumvi na beseni nikaanza kujisafisha huku nikipata maumivu makali sana.Sikwenda kabisa hospitali hadi leo hii na nilipona kwa uwezo wa Mungu baada ya mwezi kupita.Nashukuru hivi sasa nipo sehemu nzuri japo sio sana ila sio kama mwanzo.Leo nilipita ile njia ya kiwandani nikakumbuka kuleta kisa hiki.
View attachment 2484012

Pole Sana mkuu
 
Habarini ndugu wana JamiiForums,

Hivi kiwanda cha Bakharesa pale Buguruni ni uhakika kupata kazi ya kibarua ukiwa na barua ya utambulisho wa makazi?

Na hivi wanalipa kwa siku au wiki?
kuna makampuni ya kichina na ya kihindi yanafanyisha kazi watu masaa kibao na hawa machawa eti ma HR ndo wanaongoza kukandamiza watu na sheria wanazijua sheria za kazi masaa ya kufanya kazi ni saa nane na mda wa kula ukiwa hupo humo humo baada ya hapo kinachoendelea ni overtime ila kuna kampuni za kichina kuingia ni 12 alfajili kutoka moja jioni na hakuna vya overtime
 
Habarini ndugu wana JamiiForums,

Hivi kiwanda cha Bakharesa pale Buguruni ni uhakika kupata kazi ya kibarua ukiwa na barua ya utambulisho wa makazi?

Na hivi wanalipa kwa siku au wiki?
ukiwa mpemba, ndiyo
 
SITOSAHAU SIKU NILIPOTAKA KUFA PALE KIWANDANI

Ilikua mapema mwaka jana nilipitia kipindi kigumu sana baada ya kuyumba kiuchumi na degree yangu mkononi ikanilazimu kujizima data na kutafuta kazi yoyote iwe rasmi au isiwe rasmi.Nikazama zangu jf ndipo nikapata muongozo wa kwenda kiwanda cha unga kwa kurubuniwa kwamba kwa siku malipo inafika hadi buku 8 nikajipa. moyo..

Basi nikafata tafatibu zote siku ya pili nikaenda na barua ya mtendaji then nikaambiwa siku ya pili usiku nikaanze kazi.Basi bwana nikazama zangu pale mida ya saa 1 jioni nikawakuta wenzangu wapo tayari wanasubiri kuanza kazi.Wakagawa msosi pale ndani kila mtu sahani ya wali(upo kama makande) na maharage na ndizi mbivu.Kwa kua ni siku ya kwanza nikawa na uoga uoga wa kula ule msosi na niliogopa kuja kukatwa kwenye malipo[emoji28].Jamaa wakawa wananishangaa huyu msela vipi huu msosi ni lazima kuchukua haijalishi unataka au hutaki.Basi kuna jamaa akasema chukua nipe mm nitakula,wakawa wanagombania nipe mim nipe mimi.Basi nikachukua ule msosi nikampa jamaa mmoja akala na wa kwake.

Kimbembe kilianza baada ya masaa mawili viroba vilipoanza kushika toka kwenye vinu vinashuka kama mvua na vinu vipo vya kutosha mule ndani.Ili kusubiria viwe vingi ndio kazi ianze wale jamaa wakasema tuchezeni boli humu ndani(mpira wa makaratasi).Basi tukagawana huku na huku tukaanza kucheza mpira.Katika harakati za kuucheza ule mpira nikajibamiza vibaya sana kwenye kinu kipo kama upinde afu kule mbele kama wembe kwa makali yake.Ghafla bin vuu nikajikuta nipo chini nimezungukwa na watu kibao damu zinavuja kama kuku katoka kuchinjwa..Aisee nilijua leo ndio siku yangu siwezi kutoboa maana nilipasuka katikati ya kichwa.Wakaniinua pale sina hata nguvu wakasema nikapumzike pale kazi inataka kuanza.Nilishindwa coz damu zilikua zinavuja sana kuna jamaa akanielekezaa bafu akasema nikaoge ili niwe sawa.

Nilijivuta nikaenda kuoga kule bafuni maji yote yalijaa damu tu yani ili siku ilikua ndio bye bye sema Mungu hakupanga tu.Nikarudi kule ndani jamaa ndio wanagawana watu kwa makundi waanze kazi.Cha ajabu na mimi nikaitwa nikapangiwa kundi nibebe viroba.Nikawaeleza siko sawa damu zinavuja sana lakini hakuna aliyeelewa.Wakasema humu ndani ni lazima kila mtu afanye kazi.Kazi ikaanza nikaambiwa na mm nibebe kichwani zile kilo 25 kwa 50 yena viwili trip moja.Ilikua ngumu sana kubeba lakini sikua na jinsi nikajaribu tripu moja nakashindwa kichwa kilikua kinauma sana.Wakanibadilisha section wakasema niwe nawapakia watu kichwani wenyewe wanaita kijiko,yani unabeba viroba viwili pale chini na kumpa mtu kichwani.Nimefanya mara moja tu kuna jamaa akanigusa pale kichwani na kiroba basi damu zikaanza upya kutoka nikaamua kuacha nikasema liwalo na liwe cha kufia nini.

Basi nikatoka pale nikaenda nje kukaa toka ile saa 4 mpaka saa 12 asubuhi jamaa wanabeba tu vile viroba.Walikua kama 30 hivi lakini viroba walivyobeba ni zaidi ya 6,000 yani kila mmoja kama mia 2 hivi.Asubuhi ya saa 1 tukaitwa wote kwenye mgao wa pesa.Kaja kiongozi wao akasema leo kazi hamna hivyo kila mtu atapata elfu 2,aisee nilichoka mwili na akili yani kazi yote ile mtu alipwe elfu 2.Kuna watu walikua wanapinga mm kupewa ile elfu 2 kisa sijafanya kazi.Sema jamaa akanipa ile buku 2 akasema ukatibiwe.Nimetoka pale naona kama ndoto nikarudi zangu geto ile pesa nikafanya nauli sikubakiwa hata na senti..

Nimefika home kichwa chote kimeloa damu na nimepasuka vibaya sana.Sikua na pesa hivyo nikachukua chumvi na beseni nikaanza kujisafisha huku nikipata maumivu makali sana.Sikwenda kabisa hospitali hadi leo hii na nilipona kwa uwezo wa Mungu baada ya mwezi kupita.Nashukuru hivi sasa nipo sehemu nzuri japo sio sana ila sio kama mwanzo.Leo nilipita ile njia ya kiwandani nikakumbuka kuleta kisa hiki.
View attachment 2484012
Aisee hii inasikitisha sana. Pole kwa kweli
 
nimejifunza kitu Tanzania hii ukipata ajira nzuri inakulipa na mahitaji Yako yanaenda mshukuru Sana mungu....

Sent using Jamii Forums mobile app
Sana. Kuna watu shida hizi hawazijui... Juzi katika haraka ti zangu za uprofeshino winga nikakatiza pale keko viwanda I celo mpka simba oil.
Nkakutana na kijana mmoja kakosa kibarua na kula hajala hana nauli kawa mweupeee. Njaa, kiu na vumbi kafubaa. Ananiomba nauli arudi kwao vingunguti. Na mm Nina 2700 tu. Nikamuungia 200 ili nifike ninapokwenda nifike nirudi mbagala. Wakati huo nimetembea na mguu kutoka posta hadi hapo keko. Jamani mnaoweza kusaidia vijana wasaidieni japo mawazo tu. Hali si shwari huku mtaani
 
Bora hii kazi ya mwili bodi kuliko hii ya viwanda
Viwanda ni ufala kabisa kazi kubwa afu unaambulia vijisenti
 
Pana mtoto wa kichaga asubui anawahi sokoni anajumuia karoti, hoho, vitunguu, njegere, nk
Mchana ana paki mixing package yaani anaweka karoti, hoho, nk anafunga kwenye vifuko kisha anatia kwenye begi anapita mtaa kwa mtaa kuanzia saa 10 jioni. Ndani ya masaa manne mzigo wote ushaisha kwa siku hakosi elf 60 faida.
iga ufe by motivation spika
 
Mara 100 ukabebe nzege na blocks kwa siku 25,000-30,000
Zege mkuu afya. Kama inruhusu akabebe.. Mm Kwa Sasa ni Profeshino winga. Nawataftia watu maeneo yenye bidhaa za bei rahisi zaidi. Wananilipa. Nafika mpaka viwanda I. Sijui huyu mwenzagu kama ataweza. Zege mm nlibeba miaka mi 3 nyuma lakn uprpfeshino winga unanilipa sana
 
Mwanangu vip? nataka tukutane unioneshe machimbo ya bidhaa bei rahisi k/koo tusake tonge
 
Back
Top Bottom