KERO Vibarua wa Jiji la Tanga hatujalipwa malipo yetu ya mwezi Julai na Agosti

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Tunaomba wahusika wanaosimamia malipo ya vibarua katika Jiji la Tanga watulipe fedha za kazi tulizofanya katika kipindi cha Julai na Agosti.

Tunaishi kwa ugumu kutokana na gharama kubwa za maisha, huku madeni yakizidi kutuelemea. Haya ndiyo malipo tunayoyategemea kwa ajili ya kuendesha maisha yetu na kutimiza majukumu ya kila siku.

Tunaomba malipo yetu yashughulikiwe na kulipwa kwa wakati. Mnapochelewesha fedha ambazo tumeshazifanyia kazi, sisi tutaishi vipi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…