Vibonzo vya siku hizi: Ni mtindo wa kisasa au kudumaa kwa vipaji?

Vibonzo vya siku hizi: Ni mtindo wa kisasa au kudumaa kwa vipaji?

RugambwaYT

JF-Expert Member
Joined
Jan 11, 2014
Posts
1,397
Reaction score
1,899
Nimekua nikifuatiliza vibonzo kutoka kwa wachoraji mbalimbali wa siku hizi, wengi wao wanatumia picha halisi ya mhusika, then sehemu zingine za mwili ndio zinachorwa.

Sijui huu ndio mtindo wa kisasa katika uchoraji, au tuseme uwezo wa wachoraji wetu umeanza kupungua kama ilivyo kwenye sekta nyingine nyingi?

Binafsi katika uzoefu wangu wa mambo ya uchoraji, kuchora sura ya mto bila too much distortion ndio huwa the hardest part, ila other body parts ni rahisi, as all you have to do ni kuonesha ni binadamu na sio ng'ombe au paka.

Ila this new style naiona kama it's basically 'copy and paste' which most people today can easily do with their smartphones.

dodoma.jpgukawa.jpg
 
Rugambwa,

Nimefurahi sana kuona hii post yako kwasababu na mimi hivi majuzi nilistukia hii kitu na nikawaza kuwa pengine siku moja nitaizungumzia hapa JF, hivyo nimefurahi kuona nawe umeona hili na umechukua hatua ya kulileta hapa kwa kuwa naamini hawa wachora katuni wanaweza kuingia hapa wakasoma.

Kama ulivyoelezea, mimi pia nimeshangaa kuona staili yao mpya ya kivivu ya kuchukua picha halisi za kichwa cha mtu na kuunganisha na mchoro wa kiwiliwili (sjui kwanini kinaitwa kiwiliwili?, teh!)

Mimi naona ni jambo la kivivu linalorudisha nyuma taaluma yao muhimu, wanapaswa kubadilika na kujiongeza uwezo wa kuchora kama wakongwe wengine.

Wacha pia niwasifi wachora katuni wengine wengi wa hapa kwetu kwa kazi nzuri sana wanazofanya. Nimekuwa mpenzi wa katuni tangu utoto wangu (Bi.Mkora na Kingo kwenye gazeti la Majira)
Pongezi kwa:
Robert Mwampemba (katuni za Bi.Mkora)
James Gayo (Kingo)
Masoud Kipanya (Kipanya)
Mchora katuni ile ya Kabwela
Nathan skumbuki katuni yake inaitwaje.

Kila la heri.
 
K

Kweli kabisa, maana wanachokifanya ni sawa na kuchukua picha ukaweka kwenye application ya simu, afu ukajifanya umechora. Hii itaharibu sanaa hiyo saana. Maana young generation of cartoonists wanawaangalia hawa kama mwongozo wao.

Kwa hali hii hiyo sanaa tutaiharibu kabisa. Umenikumbusha hao wachoraji. Kina Macro Tibasima. Sijui hapa JF tuna mchoraji gani.
 
Back
Top Bottom