Elections 2010 Vibweka vya Uchaguzi Igunga: Mabasi kukamatwa, masanduku kwa DC na mengineyo..

Elections 2010 Vibweka vya Uchaguzi Igunga: Mabasi kukamatwa, masanduku kwa DC na mengineyo..

ITV wameonyesha mabasi ya wahuni wa CDM
 
Inaonekana CCM ubunge kwao ni deal sana ee?kwanini wanatumia nguvu kiasi hiki?
 
Inaonekana CCM ubunge kwao ni deal sana ee?kwanini wanatumia nguvu kiasi hiki?

usiwe biased, nguvu nyingi zinatumikwa kwa vyama vyote Mkuu wangu, CDM, CUF, CCM wamekodisha helkopita tena CDM yao imetumika muda mrefu zaidi, hebu fuatilia profile ya viongozi/wabunge wa vyama wanaoshinda huko.
 
attachment.php

Haya ndio mabasi manne ya nayosemekana yamekamatwa!

By the way who owns these coaster busses? Je,ni ya CHADEMA kweli au ni ya CCM lakini yamebatizwa na KUITWA MAJINA YA CHADEMA?
Watanzania siku zote tunaambiwa tu wavivu wa kufikiri na huo ndo ukweli wenyewe! Hivi hatuna WAANDISHI WA HABARI ZA UCHUNGUZI kama walivyokuwa wanafanya kina marehemu Katabalo(RIP)?

Hapa inavoonekana ni mchezo ule ule wa CCM wa kusema CHADEMA WAMEINGIZA MAKOMANDO 33 TOKA LIBYA NA AFGHANISTAN! Kama Watanzania kweli tuko serious na UHURU wetu,AMANI yetu,DEMOKRASIA yetu na UTU wetu BASI LAZIMA HII HABARI YA HAYA MABASI IWEKWE WAZI ILI WATANZANIA WAJUE NANI ANAYEFANYA UHUNI HUU WA KUTAKA KUVURUGA AMANI YA TZ KWASABABU TU YA MADARAKA. We are actually fed up.

Kamata mmiliki wa hizo coaster,madreva wake na wote waliokuwemo wapewe kibano cha uhakika ILI WATOBOE SIRI YA NANI YUKO NYUMA YA MCHEZO HUU MCHAFU. Hatuwezi kuendelea na uhuni huu sijali kama utakuwa umefanywa na CHADEMA,CCM,CUF,UWT,POLISI au yeyote yule. Watanzania tumechoka kufanywa mazezeta kwa kupewa propaganda za kishenzi za miaka ya 47!!!
 
wewe akili zako fupi kweli yani vijana wa cdm tusiende kuwadhibiti hawa wez kutegemee usalama! Hv ww uko bongo kweli?hujui hawa usalama ni usalama wa ccm?na katika billions of sh. za uchaguz igunga nao fungu lao lipo, sasa ndo tuwategemee hawa usalama kudhibiti hujuma?! Tumia akili wewe.

Yaonesha vijana wa cdm sasa mnatumia akili ndefu kujiandaa kudhibiti hata mambo ambayo si yakini!! hivi habari hizi mna uhakika ni za kweli?
Hata hivyo wote mnaishi tanzania kwa kulindwa na vyombo vya usalama vilivyo chini ya Dola kwa utaratibu unaotambulika kisheria, kinyume na hapo ni mawazo finyu kufikiri kuwa vyombo vya usalama ni kwa ajili ya CCM pekee. Vijana kwenda Nzega kuimarisha ulinzi ni kichekesho vile? Hivi kazi ya kuwahamasisha vijana wa Igunga wahakikishe wanapiga kura imewashinda?
 
Mbona wameonyesha magari tu, silaha na madawa ya kulevya viko wap?
 
Kama ulijua ccm walifanya hivyo huko mtwara ulichukua hatua gani za kisheria?

Kama hajachukua hatua yeyote ile unaonaje ukiambiwa kuwa wewe ni mtengenza majungu na fitna ili kuleta vurugu ktk demokrasia?

CDM mlishindwa nini kuweka mawakala waaminifu?

CCM = DOLA
CCM = UCHAKACHUJUAJI. Unategemea haki gani?
 
CCM kura hizo za wizi huwa wanapeleka kwenye eneo la kukusanyia masanduku hasa kwa wakurugenzSi wa halmashauri,na watu wakizubaa tu kidogo karata zinachanganywa na wanatangaza kutokana na walivyo chakachua.
Sawa kabisa. Ni vigumu sana kutendeka wizi kwenye vituo vya kupiga kura, kwahiyo nafasi pekee inayotumiwa na CCM ni kwenye maeneo ya kukusanyia masanduku ambapo kura zilizowekewa alama ya mgombea wao zinapelekwa kisha kuingizwa kijanja na makuwadi wa CCM. Zamani walimu walikuwa wakitumika lakini baada ya mfarakano baina ya waalimu na JK sasa wanawatumia polisi, Usalama wa Taifa na hata JWTZ kama tulivyoshuhudia katika uchaguzi uliopita. Eti magari ya Polisi na JWTZ ndiyo yalikuwa yakikusanya masanduku kana kwamba nchi iko katika hali ya kivita. Ukweli huu unafafanua ni kwa nini CCM wanapoinga mabadiliko katika sheria za uchaguzi. Wilayani kunakuwa na "Returning" Officer ambaye kwa kawaida ni kibaraka wa CCM na mtumishi wa serikali eti ndiye pekee mwenye haki ya kuAtangaza matokeo ambayo mara nyingi hayalingani na idadi halisi ya kura wapinzani walizopata. CHADEMA wakatae kabisa kura zao kubebwa bila kusindikizwa na watunze nakala halisi zilizosainiwa na mawakala wote katika kila kituo. Tukiwa smart katika hili CCM wamekwenda na maji.
 
Yaonesha vijana wa cdm sasa mnatumia akili ndefu kujiandaa kudhibiti hata mambo ambayo si yakini!! hivi habari hizi mna uhakika ni za kweli?
Hata hivyo wote mnaishi tanzania kwa kulindwa na vyombo vya usalama vilivyo chini ya Dola kwa utaratibu unaotambulika kisheria, kinyume na hapo ni mawazo finyu kufikiri kuwa vyombo vya usalama ni kwa ajili ya CCM pekee. Vijana kwenda Nzega kuimarisha ulinzi ni kichekesho vile? Hivi kazi ya kuwahamasisha vijana wa Igunga wahakikishe wanapiga kura imewashinda?
mkuu ni kweli vyombo vya usalama ndo vinavyostahili kushugurikia tuhuma hizo, lakini utafanya nini kama vyo hivyo ndio vinavyo ratibu hizo tuhuma?. Bwana Rweyemam unaishi tanzania?
 
Hiki kirusi kinachojiita FaizaFoxy ni cha hatari kuliko kile cha ukimwi na kimeta! Ni kirusi pandikizi-haramu! Inaonekana kila habari inayotoka humu chenyewe kinajaribu kupachika mianya ya udini tu! Hiki ni kirusi kilichosheheni roho ya fitina ya jini Makata na Maimuna na kilichojaa harufu chafu ya udini!
 
mkuu ni kweli vyombo vya usalama ndo vinavyostahili kushugurikia tuhuma hizo, lakini utafanya nini kama vyo hivyo ndio vinavyo ratibu hizo tuhuma?. Bwana Rweyemam unaishi tanzania?

Mkuu yawezekana ni kweli lakini ukiangalia wakati huu wa teknohama ambapo habari, picha na taarifa vyaweza kusambazwa kwa muda mfupi nashindwa kuamini kama kweli tuhuma hizi zinazoripotiwa zina ukweli wa kujiridhisha kwamba vitendo hivi vipo!!. Mambo mengine ni ya ajabu kidogo!, picha za mabasi kama haya ya Mukesh zimepigwa lakini kama kungekuwepo na vitu vinavyohisiwa natumaini vingepigwa picha pia na tuoneshwe hapa jamvini...
 
Yaonesha vijana wa cdm sasa mnatumia akili ndefu kujiandaa kudhibiti hata mambo ambayo si yakini!! hivi habari hizi mna uhakika ni za kweli?
Hata hivyo wote mnaishi tanzania kwa kulindwa na vyombo vya usalama vilivyo chini ya Dola kwa utaratibu unaotambulika kisheria, kinyume na hapo ni mawazo finyu kufikiri kuwa vyombo vya usalama ni kwa ajili ya CCM pekee. Vijana kwenda Nzega kuimarisha ulinzi ni kichekesho vile? Hivi kazi ya kuwahamasisha vijana wa Igunga wahakikishe wanapiga kura imewashinda?

Nina wasiwasi na Tanzania unayoishi. NAKUHAKIKISHIA KWA UMRI WANGU NA UZOEFU WANGU SERIKALINI (37 YRS) katika mafanikio makubwa ambayo CCM walifanikiwa ni kuvuruga majukumu ya dola na kuyafanya ni majukumu yao. Kwa hiyo vyombo vyote vya dola ni matawi ya CCM. (Rejea kanda za matawi ya chama).

Mikakati hasa ya CDM inaonekana kama ni ubabe ubabe, uongo, uasi na vurugu. Muono huo unatoka na pesa nyingi kutumika na CCM ili ionekane hivyo. Kwa jinsi baadhi mmedumamzwa na mbinu chafu za CCM, inafikia hamuamini kinachotokea.

Ebu jielimishe kidogo kwa nini wana CCM kwa kutumia rasilimali zetu wote wapo Igunga na wanashinikiza left and right kuwabughudhi wananchi na wapinani wao? Ni sababu kubwa moja wananchi HAWATAKI, ila kwa sababu wao ni dola wanashikiza kwa magumashi na kujitangaza kuwa wanapendwa.

Kama uonavyo hiyo picha haina ujumbe wo wote. HIYO NDIYO DOLA kinachotakiwa ni kukuaminisha kimagumashi kwa matarajio kuwa hutauliza wala huna uwezo wa kufikiri zaidi ya kuona hayo mabasi hata kama yana haki yakuendelea na shughuli zake za kawaida. Usije kuja shangaa kwamba mmiliki ataandamwa pia.
 
Mimibaba,

Hakika umenena baba. Yote ni ukweli mtupu. Big up!
 
kuna mawakala wa vyuo vikuu wenye simu za mawasiliano ya internet so kila kituo wapost matokeo ya uchakuzi kwenye kila kituo na jf tujtaumlishe na kwa mara ya kwanza jf tutatangaza mshindi wa ubunge na kama tume wakitangaza wa kwao basi wamtafutie jimbo maalum la kuongoza na si IGUNGA
 
Back
Top Bottom