Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 301,577
- 754,412
Naumia sana ninapomuona mtu mwenye matatizo ya akili'(ufahamu), wengine huita vichaa ama wendawazimu. ... Baadhi yetu tuna tabia ya kuwafukuza na wakati mwingine kuwapiga kabisa.
KUMBUKA! Hawa nao ni binadamu wenye ndugu jamaa na marafiki! Wengine wana watoto... Ni jambo la kijamii linalohitaji tafakuri ya kina kwakuwa ni wachache MNO walizaliwa wakiwa vichaa.... Hujafa hujaumbika!!!!
Turejee kwenye mada yetu! Vichaa wako wa aina tofauti wapole waoga wakorofi wababe micharuko nknk.... Yote kwa yote hufanya vitu tofauti na kawaida yaani hutenda kinyume na mazoea.
Kuna dunia ya vichaa! Kuna mawasiliano kati yao na vitu tusivyoviona sisi lakini wao wanaviona kusikia na hata kuhisi
Huwa tunasema nut zimelegea ama dish limecheza au tunawaita dakika tatu mbele.
Nut zikilegea kwenye gari ama mashine lazima kutatokea sauti za ajabu.Dish likicheza lazima hutapata picha clear.
Dakika tatu mbele manake hii ni foreseen.. Yani wanaona kabla ya wakati husika kufika... [emoji15] [emoji144] je hiki ndio chanzo cha uchizi wao?
Wanapokaa na kuongea pekeyao kwa mtazamo wetu... Naamini hawaongei pekeyao bali huwa na mawasiliano na viumbe visivyoonekana kwa macho yetu.
Kuna viwango vya ukichaa! Mtu hawezi kuwa kichaa kwa asilimia mia moja! Na ikitokea akawa hivyo hachukui round anakufa
Lazima kuna asilimia za ufahamu hubakishiwa.
Ndio maana hasahau kula
Ndio maana mwili ukichoka atapumzika
Ndio maana usiku ukiingia atalala
Ndio maana hachani hela wala kutupa
Ndio maana akivuka barabara lazima achukue tahadhari japo si kwa asilimia mia moja
Ndio maana huhisi kupendwa ama kuchukiwa nknk

Yote kwa yote kuna jambo kubwa nyuma ya vichaa ambalo huwa hatujishughulishi nalo zaidi ya kuwa na mawazo hasi kila tuwaonapo!