Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mwanamuziki wa zamani na mbunge Vicky Kamata baada ya ndoa yake kudaiwa kuzuiliwa kufungwa kutokana na kudaiwa kubainika kuwa mwanaume aliyetaka kufunga naye ndoa ana ndoa nyingine, amefunguka kwa kudai kuwa hizo zilikuwa ni habari za kutungwa. Vicky Kamata ameiambia amplifaya ya Clouds fm jana kuwa maneno mengi ambayo yalikuwa yanazungumzwa kuhusu ndoa yake kutofunga yalikuwa yametengenezwa na watu. Kweli ni maradhi kama ambavyo ilitangazwa wakati huo, lakini pamoja na hayo mimi bado nasema mungu alikuwa hajapanga ,alikuwa ajaruhusu kuwa tarehe 24 mwezi wa tano iwe siku wa kufunga ndoa, mimi kama binadamu na mwenzangu tulipanga lakini mungu alipanga vinginevyo, kwaiyo siku zote mapenzi ya mungu huwaga yanatimia siyo mapenzi ya binadamu.
Ni kweli alishawai kufunga ndoa lakini ninachofahamu mimi ni kwamba waliachana kihalali kabisa kwa divorce ya mahakama ya Kinondoni mwaka 2012 na mimi siyo mtoto mdogo kwamba ninaweza mpaka nikafikia hatua hiyo bila kuwa nimemchunguza huyo mtu, kuhusu swala la kwamba alikuwa na mke wake , mke wake alikwenda kuzuia Kanisani sijui alikuja Bungeni, yale yalikuwa tu ni maneno ambayo yalitengenezwa na baadhi ya watu kwa interest
zao ,lakini siyo kwamba nilikuwa nimeingilia ndoa ya mtu ata kidogo, kwa sababu ata huyo mke wa kwanza wa huyo aliyekuwa mchumba wangu
aliongea na vyombo vya habari akasema mimi sijaenda Dodoma wala sijaenda kuzuia harusi, kwaiyo maneno yaliyokuwa yamezagaa ,sijui mke wake amezuia yalikuwa ni maneno ya kutengenezwa na watu tu kwa nia zao wenyewe lakini siyo kweli.
Kuhusu kwamba ajulikani alipo mimi hilo siwezi kumjibia, mimi nafahamu kwamba yupo na anaendelea na shughuli zake kama kawaida, kama ambavyo
mimi naendelea na shughuli zangu kama kawaida, tunawasiliana, yani cha kufahamu tu kwamba ndoa haikufungwa basi, hata kama kuna mkono wa binadamu katika jambo hilo mimi naamini mungu ndo mwenye mamlaka na Mungu ndiyo mwenye kupanga mambo, kwaiyo kama Mungu alikuwa anataka hiyo harusi ifugwe ata kama kungekuwa na binadamu mwingine hataki bado ingefungwa, kwaiyo mimi sitaki kuamini sana kwamba kuna waheshimiwa wabunge wenzangu wamechangia kwa kiasi kikubwa kwamba ndoa ile isifungwe, mimi ninaamini ni mapenzi ya Mungu tu yametimizwa kwa staili hiyoAlisema Vicky
Huyu tayari Miles-gauge imesoma saana , na bado wa-kulu waendelea kubutua..sasa nani abebe huo mzigo? Ana watoto wawili..kwanini hao baba watoto..asiamua mmoja kufunga nae ndoa? Sio bure..ana kasoro huyu mwanamke!
huyo aliyekuwa mchumba wangu? du hii sentensi inamaana gani? kwani sasa sio mchumba wake?
Pole mwaya najua inauma, ila acha uwongo haiwezekani ndoa ikaachwa kufunga bila sababu ya msingi; eti kuumwa no way. Wakati mwingine tunmsingizia Mungu eti mapenzi ya Mungu! Umesema "aliyekuwa mchumba wangu' kwa hiyo sasa hivi sio mchumba tena? Kitu gani kimesababisha useme "aliyekuwa mchumba wangu" usiseme " mchumba wangu" embu funguka mama.
Ningekuwa mimi nisingeongea Ngo"do! unavyoongea ndivyo unavyozidi kuwapa watu maswali na kuendelea kusema wenyewe tulishasahau , tupo kwa Komba sasa unaturudisha nyuma lol!Mwanamke Tulia
Hatafuti mume? Nimejitokeza
Kumbe ndio maana na avatar ukabadilisha...nimekushtukia....te te te; kwa sura hiyo subiri PM
Huyu tayari Miles-gauge imesoma saana , na bado wa-kulu waendelea kubutua..sasa nani abebe huo mzigo? Ana watoto wawili..kwanini hao baba watoto..asiamua mmoja kufunga nae ndoa? Sio bure..ana kasoro huyu mwanamke!