Vicky Kamata afunguka kuhusu ndoa yake

Vicky Kamata afunguka kuhusu ndoa yake

huyo aliyekuwa mchumba wangu? du hii sentensi inamaana gani? kwani sasa sio mchumba wake?
 
Mwanamuziki wa zamani na mbunge Vicky Kamata baada ya ndoa yake kudaiwa kuzuiliwa kufungwa kutokana na kudaiwa kubainika kuwa mwanaume aliyetaka kufunga naye ndoa ana ndoa nyingine, amefunguka kwa kudai kuwa hizo zilikuwa ni habari za kutungwa. Vicky Kamata ameiambia amplifaya ya Clouds fm jana kuwa maneno mengi ambayo yalikuwa yanazungumzwa kuhusu ndoa yake kutofunga yalikuwa yametengenezwa na watu. “Kweli ni maradhi kama ambavyo ilitangazwa wakati huo, lakini pamoja na hayo mimi bado nasema mungu alikuwa hajapanga ,alikuwa ajaruhusu kuwa tarehe 24 mwezi wa tano iwe siku wa kufunga ndoa, mimi kama binadamu na mwenzangu tulipanga lakini mungu alipanga vinginevyo, kwaiyo siku zote mapenzi ya mungu huwaga yanatimia siyo mapenzi ya binadamu.

Ni kweli alishawai kufunga ndoa lakini ninachofahamu mimi ni kwamba waliachana kihalali kabisa kwa divorce ya mahakama ya Kinondoni mwaka 2012 na mimi siyo mtoto mdogo kwamba ninaweza mpaka nikafikia hatua hiyo bila kuwa nimemchunguza huyo mtu, kuhusu swala la kwamba alikuwa na mke wake , mke wake alikwenda kuzuia Kanisani sijui alikuja Bungeni, yale yalikuwa tu ni maneno ambayo yalitengenezwa na baadhi ya watu kwa interest
zao ,lakini siyo kwamba nilikuwa nimeingilia ndoa ya mtu ata kidogo, kwa sababu ata huyo mke wa kwanza wa huyo aliyekuwa mchumba wangu
aliongea na vyombo vya habari akasema mimi sijaenda Dodoma wala sijaenda kuzuia harusi, kwaiyo maneno yaliyokuwa yamezagaa ,sijui mke wake amezuia yalikuwa ni maneno ya kutengenezwa na watu tu kwa nia zao wenyewe lakini siyo kweli.


Kuhusu kwamba ajulikani alipo mimi hilo siwezi kumjibia, mimi nafahamu kwamba yupo na anaendelea na shughuli zake kama kawaida, kama ambavyo
mimi naendelea na shughuli zangu kama kawaida, tunawasiliana, yani cha kufahamu tu kwamba ndoa haikufungwa basi, hata kama kuna mkono wa binadamu katika jambo hilo mimi naamini mungu ndo mwenye mamlaka na Mungu ndiyo mwenye kupanga mambo, kwaiyo kama Mungu alikuwa anataka hiyo harusi ifugwe ata kama kungekuwa na binadamu mwingine hataki bado ingefungwa, kwaiyo mimi sitaki kuamini sana kwamba kuna waheshimiwa wabunge wenzangu wamechangia kwa kiasi kikubwa kwamba ndoa ile isifungwe, mimi ninaamini ni mapenzi ya Mungu tu yametimizwa kwa staili hiyo”Alisema Vicky

Mmmmh nahisi bado Mbunge Vicky anaumwa wampime vizuri, Yani Ndoa ifungwe kanisani wakaachane mahakamani nawewe ukubali useme walipeana taraka????Uyo bado mume wa mtu hadi mkewe afe na si mahakama kuvunja, Nakushauri Tafuta wako dada Mbunge!!
 
Huyu tayari Miles-gauge imesoma saana , na bado wa-kulu waendelea kubutua..sasa nani abebe huo mzigo? Ana watoto wawili..kwanini hao baba watoto..asiamua mmoja kufunga nae ndoa? Sio bure..ana kasoro huyu mwanamke!
 
Huyu tayari Miles-gauge imesoma saana , na bado wa-kulu waendelea kubutua..sasa nani abebe huo mzigo? Ana watoto wawili..kwanini hao baba watoto..asiamua mmoja kufunga nae ndoa? Sio bure..ana kasoro huyu mwanamke!

Bonge la papuchiii yaaani oil seal Zimelegea kabisaaa sasa nani ataoa
 
Pole mwaya najua inauma, ila acha uwongo haiwezekani ndoa ikaachwa kufunga bila sababu ya msingi; eti kuumwa no way. Wakati mwingine tunmsingizia Mungu eti mapenzi ya Mungu! Umesema "aliyekuwa mchumba wangu' kwa hiyo sasa hivi sio mchumba tena? Kitu gani kimesababisha useme "aliyekuwa mchumba wangu" usiseme " mchumba wangu" embu funguka mama.

Naungana nawe unakuta Mungu analaumiwaaa!
 
Drama in ze city!!!tumewachoka, mie nataka tanganyika yetu
 
Ningekuwa yeye wala.kusema.public nisingesema.
 
Au angenitafuta nimwandikie speech...maana amejikanganya kuliko hao 'waliomzushia'...

Jamani kama unachoongea hakina ukweli ni heri ukae kimya...hakuna kitu kigumu kama interview kama huna uzoefu wa kujibu maswali...hapa Vick amejimaliza mwenyewe...

Ndio maana utasiki kampuni inakwambia weka maswali yako kimaandishi; si wajinga wanaogopa kutoa siri bila kujua endapo wataruhusu interviews...

Ningekuwa mimi nisingeongea Ngo"do! unavyoongea ndivyo unavyozidi kuwapa watu maswali na kuendelea kusema wenyewe tulishasahau , tupo kwa Komba sasa unaturudisha nyuma lol!Mwanamke Tulia
 
Siasa mpaka kwenye ndoa? Naomba mwongozo wa spika
 
Dulayo anasema ''chezea vijana wa mujini wewe..?? Utakoma mwenyewe!!" Bwn harusi mjanja mjanja hasomeki bibie kazama gents....!
 
Huyu Dada Muongo aseee!!!

Sasa mbona mchumba hakwenda kumtembelea kipindi yuko Hospital??

Anaendelea na Shughuli zake..Tunawasiliana...Haya ni majibu ya kisiasa ..Afadhali angekaa kimya
 
Huyu tayari Miles-gauge imesoma saana , na bado wa-kulu waendelea kubutua..sasa nani abebe huo mzigo? Ana watoto wawili..kwanini hao baba watoto..asiamua mmoja kufunga nae ndoa? Sio bure..ana kasoro huyu mwanamke!

yani umeona ikulu yetu ni pango la makahaba?
 
Kanisa Katoliki halitambui talaka ya kuvunja ndoa iliyokwisha fungwa Kanisani....Kanisa halivunji ndoa bali ktk mazingira fulani baada ya juhudi za usuluhishi kushindikana ni kuwatenganisha (si kuvunja) na hapo hakuna kushiriki tendo na mtu mwingine labda upatane na mweza wako wa ndoa.Kifo pekee ndicho kina maliza uhai wa ndoa na hilo lilifafanuliwa pia na paroko ktk kanisa kulikopangwa kufungwa ndoa ya vicky.Nadhani Vicky awe honest tu kuwa aliingizwa chaka na hakujua.Wote ni binadamu na makosa ndio sifa yetu kuu asijali yote maisha tu....
 
Back
Top Bottom