Amesema kiongozi wa awamu ya tano (jiwe) alikuwa mtu katili sana kiasi cha kumfanya apate taabu sana.
Amewasihi watanzania kuishi kwa kutenda mema maana duniani tunapita. Jiwe alilewa madaraka.
Amemaliza kwa kusema pamoja na kufuta andiko lake la kumshutumu jiwe ni kweli jiwe aliniumiza sana.
Source: StarTv (Medani za Siasa) muda huu.
==========
Mwandishi: Hujaeleza mheshimiwa Vicky Kamata, umezunguka sana. Swali la msingi, ni kitu gani kigumu ama ni jambo gani, wakati gani ambao ulikumbana na jambo gumu ambalo ukitafakari unaona kabisa kidogo likutoe kwenye reli?
Vicky Kamata: Unazungumza wakati tayari niko bungeni au wakati natamani kuwa kwenye siasa?
Mwandishi: Tayari uko kwenye siasa
Vicky Kamata: Nikiwa bungeni, labda kile kipindi ambacho awamu ya tano iliingia, mimi ilikuwa tayari ndio nimeolewa, nina ndoa changa tu ikatokea bahati mbaya, siwezi kusema bahati mbaya, mwenye ofisi yake akisema pumzika nataka huyu akae hapa utalalamika? Huwezi kulalamika.
Hicho kilitokea kwa mume wangu, alikipokea very positively, binafsi nilikipokea kawaida kabisa na maisha yakawa mazuri kabisa lakini sasa wenzangu pale bungeni wakaanza kama kunitenga.
Chochote ninachoshauri naonekana ninashauri kwa sasabu nina hasira, kitu ambacho sikuwa nacho wala sikiwazii kwasababu mhusika mwenyewe hajalalamika, walihusisha kazi ya mume wangu na kazi yangu.
Tena wanaCCM wenzangu mpaka walikuwa wanachangia wazi kabisa yaani flani, anakupiga kijembe cha wazi kabisa kwamba una hasira, mume wako ametumbuliwa.
Mwandishi: Umekuwa mbungewa viti maalum kwa miaka 10 mkoa wa Geita, kwanini ukaja huku(Dar-Kibamba) ambako hukufanya chochote kwa ajili yao? Hofu yako ilikuwa nini Geita?
Kamata: Sikuwa na hofu isipokuwa katika majimbo yote ya Geita, yote yalikuwa na wabunge ambao ni wazuri, kaak zungu na wanafanya kazi nzuri kiasi huoni sababu ya kwenda kusukumana na Dotto Biteko, Kanyasu au uende kwa Msukuma
Mwandishi: Kwa mantiki hiyo unataka kutuambia Kibamba hakukuwa na mbunge anayefanya vizuri?
Kamata: 'Exactly' mimi ni CCM mbunge aliyekuwepo wakati ule alikuwa ni wa upinzani na niliona ilikuwa ni wakati sahihi wa kurudisha jimbo letu kwenye chama cha mapinduzi, Kibamba nilienda kwasababu jimbo lilikuwa upinzani na kule kwetu hakuna jimbo lolote lilikuwa upinzani, majimbo yote yalikuwa ni CCM na yalikuwa na wabunge wanapendwa
Mwandishi: Unataka kuwaaminisha watanzania, majimbo ambayo yanaongozwa na wabunge wa CCM ndio yanayopofanya vizuri
Kamata: Sijasema hivyo, inawezekana yapo majimbo ya wabunge wa CCM na hayafanyi vizuri lakini kwa mkoa wangu wa Geita wana sifa nzuri na wanafanya kazi nzuri.
Mwandishi: Ni kweli kwamba wanawake wengi walioko kwenye siasa wanatumika kwenye rushwa ya ngono?
Kamata: Mimi kama mbunge wa viti maalum nilipigiwa kura na wanawake wenzangu, sasa ukiniambia kuna rushwa ya ngono sijui hata inakuwaje lakini sidhani, siwezi kulijibia hilo.
Mwandishi: Hivi karibuni tulishuhudia andiko lako katika mitandao ya kijamii ambalo liliibua hisia za watanzania na nikiona kila mmoja akiipost kwa walichodai umetoa povu, nini ilikuwa dhamira ya andiko lako?
Kamata: Ningeshangaa usingeniuliza hilo swali, dhamira ya andiko langu ilikuwa ni kukumbusha watanzania wenzangu au mtu yoyote ambae angepita kwenye 'page' yangu kwamba hapa duniani sio mahali petu pa kudumu, tujitahidi kusihi vizuri ili tutakapoondoka tuache historia nzuri kwasababu hakuna atakaebaki hapa, hapa tumepewa muda mchache tu lakini katika muda huu mchache tuyafanye yale mzee Mwinyi amekuwa akituambia, kwamba maisha ni hadithi tu.