Ni kilio kilichokuwa kikitutesa wengi kwa muda mrefu, yani kupata kadeti original ilikuwa ni shughuli pevu, tushapigwa za uso mara kadhaa kununua kadeti za elf 40 tukidanganywaa kwamba ni original. yaani walioweza kununua kadeti original za dukani walikuwa ni wale daraja la juu zaidi kiuchumi, ama wenye connection za nje, wengine tulishakariri vibanda vya mitumba wanakouza kadeti za dickies.
Kwa sasa ukinunua vucobss ni mkataba, Sehemu nilipo ni mkoani natokwa elf 40 lakini sijutii pesa nayoitoa, najua napata kitu quality kitachodumu na ni kipya.