The Dictator
JF-Expert Member
- Jul 20, 2018
- 4,475
- 12,281
Jamaa anaitwa Victor Lustig mzaliwa wa nchi ya Ufaransa. Alijulikana sana kama “mtu aliyeliuza Eiffel Tower” na cha kushangaza zaidi, alijaribu kulifanya tukio hilo mara mbili.
Mwaka 1925, Lustig alijifanya kuwa afisa wa serikali ya Ufaransa na kuwaambia wafanyabiashara wa chuma chakavu kwamba serikali ilikuwa imeamua kuibomoa Eiffel Tower na kuuza vyuma vyake kutokana na gharama. Kwa ustadi mkubwa aliandaa nyaraka bandia na hata akawapeleka wanunuzi kuugua mnara huo.
Baada ya wafanyabiashara kadhaa kujitokeza kuununua, alimshawishi mfanyabiashara mmoja aitwaye André Poisson kwamba ameshinda zabuni na mnara unaweza kuwa wake.
Poisson hakutaka kuchelewa kabisa akaona fursa sindio hii!? akamlipa Lustig fedha nyingi pamoja na rushwa ili amchaguliwe kama mnunuzi pekee. Baada ya malipo kukamilika Lustig akatoroka na fedha hizo mpaka mafichoni vienna nchini Austria.
Poisson alipoona ametapeliwa na ukweli ni kwamba mnara ule haukuwa ukiuzwa aliona aibu sana kiasi kwamba hakuripoti utapeli huo polisi. Lustig akiwa Austria alifuatilia magazeti ya Ufaransa kuona kama Poisson ameripoti utapeli huo. Lustig alipogundua kuwa hakuna habari zozote za kukamatwa kwake, akaamua kurudi Paris na kujaribu kuuza Eiffel Tower tena kwa mara nyingine.
Safari ya pili haikuenda nzuri; mnunuzi aligundua kuwa kuna utapeli mahali na polisi wakaingizwa, hivyo Lustig akatoroka tena, safari hii akaelekea Marekani kumalizia pensheni yake iliyobaki.