- Tunachokijua
- Madai
Mtumiaji mmoja wa Facebook alichapisha taarifa kueleza kuwa Victor Mhagama ambaye ni mtoto wa Jenista Mhagama ambaye ametengazwa kushinda kura za maoni katika jimbo la Permiho
Uhalisia wa madai hayo
JamiiCheck imefuatulia na kujiridhisha kuwa Taarifa hiyo si ya kweli na haijachapishwa na chanzo chochote kuaminika.
Afisa Uhusiano wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Doreen Kapwani amesema “Taarifa hiyo siyo ya kweli, hakuna ukweli wowote kuhusu hilo.”
Awali, Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Ruvuma, Hamza Mwenda alisema wamempa wito wa kufika Ofisi za TAKUKURU, Victor Mhagama ambaye yupo kwenye mchakato wa kuwania Ubunge kupitia CCM katika Jimbo la Peramiho ili kuzungumza naye na si kweli kwamwameshazungumza naye au wamemkamata.