Samatta kama angepataga nafasi ya kwenda ulaya kipindi akiwa na umri wa miaka 18 hivi, angekuja kuwa tegemeo sana katika nchi yetu, ukweli ni kwamba kwa umri alionao sasa ni vigumu sana kwenda nje na kufanya vizuri, kwakuwa kuna miaka kadhaa ya kuzoea ligi husika na mazingira, kwa umri alionao sasa kwa wachezaji wa ulaya hapo anakuwa kaishajulikana uwezo wake na anaendelea kujifundisha mambo machache ili yamsaidie! ila kwakuwa ana kiu ya kwenda nje pia anaweza kwenda na akajitahidi kung'aa ndani ya muda mfupi kwakuwa ana nia ya dhati ya kucheza ulaya..! Mimi kama mtanzania natamani nione mtanzania ktk ligi za nje hivo kwanini asiwe samatta...! Dua zangu unazo kijana wetu we komaa tu