JK Mrisho yupo vizuri sana katika lugha ya queen Elizabeth. Dunia sio kijiji bali global wise na ivo hakuna jinsi yoyote ile tunaweza kuiepuka lugha ya kiingereza (internatinally accepted world wide language). If yiu cannot speak and utter English language is better you keep quiet.
Eti mtu umezaliwa na kulelewa usukumani halafu unaongea Kisukuma cha kuungaunga!
Eti umekulia na kukomaa nchini Tanzania toka utotoni halafu Kiswahili unaongea cha kuungaunga!
Eti umesoma hadi kutunukiwa UPhD kwa lugha ya malkia halafu unaongea Kimombo cha kuungaunga!
Umekuwa waziri kwenye serikali tofauti kwa miaka zaidi ya ishirini halafu hujui taifa lilifikaje ilipo!
Kweli? Hapo lazima utakuwa kilaza wa kutupwa lakini kwa ujuha wako ukajiaminisha wewe ni genius!
Matokeo yake ndio hayo tuliyoshuhudia kwa mwendazake…ujeuri, ukatili na chuki zinatawala moyo wako.
Na zinatumika kama kinga yako dhidi ya wenye akili zaidi yako katika jitihada za kuficha mapungufu yako.
Ghafla na bila kutegemewa haupo, unakufa na kufutika katika uso wa dunia na kuwaacha wafuasi wako yatima.
Huko ahera unaungana na vilaza wenzako mnaofanana na kuchungulia yanayojiri duniani mlikotoka.
Mnajuta…! Laiti mngejua…