Video: Angalia Bodaboda alivyogongwa na Mwendokasi

Umetumia hisia hapa,ila ukweli ni kwamba dereva wa mwendokasi hapo hana makosa
 
Sawa mkuu nimekusoma ila nashauri yawekewe hono ya Treni ili linapokaribia kwenye makutano lipige honi ikibidi lisimame kwa muda wa sekunde tatu hata kama mataa yameruhusu
 
Mama ananikataza sanaaa kupanda bodaboda!
Kuanzia sasa namsikiliza[emoji119]
Nimewahi kukoswa na Rav 4 moja pale mataa ya External ilikuwa mida ya saa 6 mchana sitosahau na ndio mwisho wangu kupanda Boda. Ilikuwa 2018. Hapo natokea Ubungo naenda Airport, taa zilikuwa nyekundu na ziliruhusiwa gari zinatokea kushoto kwa maana ya Mabibo, kama kawaida Boda akapenya kwenda mbele nikijua kama kawaida anaenda kusimama kumbe anapitiliza aisee, baada ya kuvuka hapo kusogea mbele kidogo akakutana na guta linakatisha kidogo tena tujae. Nilimwambia uliponifikisha panatosha nikampa 2k. Nikatafuta mwingine. Nilikoma aisee.
 
Mwendo Kasi Hana kosa Wala hastahili lawama!.
Huyo bodaboda ni kama kajiua mwenyewe!
Tatizo la bodaboda wengi hawajaenda driving schools kwahiyo wanachojua ni kuvuta moto na kupangua gia tu kama vile wapo majangwani ambapo hakuna watumiaji wengine wa Barbara. Sheria za usalama barabarani zinakataza mtu kuendesha chombo Cha moto akiwa amelewa au akiwa na uchovu mwingi unaoweza kumsababishia usingizi akiwa barabarani lakini naamini wapo bodaboda wanaokunywa hizo K Vanti na vilevi vingine wakiwa kazini hapo wanaweza gongwa hata na malori sio lazima mwendo Kasi.
 
Boda nae hata kuchungulia, yani kajaa barabarani na speed ileile. Hata kama ingekuwa barabara ya kawaida kwa gari yoyote huyo boda angepata ajali. Kajisahau kuwa kuna watumiaji wengine achungulie kidogo.
Noda wajifunze kuwa makini kwenye maeneo ambayo yanahitaji kutoa kipaumbele kwa wengine. Hapo wala hakuna haja ya taa za kuongozea magari.
 
Uendeshaji wa pikipiki unaonekana kama ni rahisi sana,lkn pamoja na urahisi wake kunahitajika elimu kubwa sana juu ya usalama wake...
Boda boda wengi hawana leseni Wala hawajapata mafunzo ya udereva. Mtu kafundishwa kuendesha pikipiki huko mtaani kwao tayari anaingia barabarani kubeba abiria. Ilikuwa Kuna haja kabla ya kupanda pikipiki kumwambia dereva akuonyeshe leseni ya udereva na cheti Cha udereva.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…