"mdahalo" maana yake nini? Nilidhani ni lazima mdahalo ukwaanishe pinzani mbili na zaidi.
Huu ni mkutano wa mchungaji na wana kwaya, wakihutubiwa neno la uzima ambalo tayari walishalipokea. Maswali karibu yote yalianza na "ndugu rais mtarajiwa, utafanya nini ikulu..." sasa kama umeshaamua huyu ndio unataka awe rais, umekuja kumhoji wa nini?
Slaa anakubali kusaidiwa majibu na mratibu wa 'mdahalo' ambae ni choka mbaya, slaa akiulizwa kitu mwanamke anawahi "swala la mgombea binafsi halimo kwenye ilani ya chadema... Swala la elimu limeshaongelewa." kwa hiyo kwenye elimu slaa akishasoma ilani ya chama basi kamaliza, hakuna maswali! Na swala halimo kwenye ilani kwa hiyo tusiliongelee, kwa hiyo ningeuliza, je, bwana slaa maadili yako yanaonekaje mbele ya shutuma za ugoni na mke wa mtu, utanambiaje, ugoni wa slaa hauko kwenye ilani ya chama, usiliongelee!
Na mwenyekiti wa chama yuko mbele kakaa mkao wa picha, badala ya kumwacha mgombea wao mbele awe kivutio cha kati cha mkutano wao.
"mdahalo" ulikaa kijinga jinga fulani.