Sidhani kama ni kweli, itakuwa anachafuliwa, labda ile ya kifua wazi. Lakini tujifunze jambo moja, si vizuri kushiriki kumchafua mtumishi wa Mungu, tusisahau ana watu wengi waliomuamini Kristo kupitia yeye. Mimi ni Mkatoliki lakini natambua nafasi ya mtumishi yeyote wa Mungu hata kama si dhehebu langu. Tukumbuke habari za Nuhu kwenye mwanzo 9: 20-23 jinsi alivyolewa hadi kubakia uchi, mtoto wake wa kwanza alivyomuona akaenda kuwaambia wenzake na mmoja wao ndio akaenda kumfunika. Yule mtoto aliyeshindwa kumsitiri baba yake alilaaniwa! ( hapo kwa dunia ya sasa tungemuona huyo mzee mdhambi kwa kunywa pombe! lakini maandiko yanaonesha laana ilikokwenda). Usishiriki kumchafua mchungaji Gwajima maana haitokuongezea au kupunguza kitu. Heshimu utu wake.