Video: DIAMOND aionyeshea serikali kidole cha kati, aimba tena NYEGEZI

Kwameh

JF-Expert Member
Joined
Dec 3, 2011
Posts
1,793
Reaction score
2,152


Biashara inapokuwa kubwa, makampuni huwa yanaanzisha kitengo kinaitwa compliance department na huajiri wataalam wa kuhakikisha biashara haibughudhiwi bugudhiwi na serikali kwa kuvunja vunja visheria vidogo vidogo na vikubwa.

Diamond jana, Desemba 15, akiwa Mwanza kaimba tena "mambo ya Amber Rutty." Mkuu wa BASATA katoa tamko la dharura kwamba ameyasikia, yuko njiani Arusha atarudi makao mkuu kumshushia rungu zito kwa sababu Diamond amedharau baraza, wizara na serikali yote kwa kuimba mambo ambayo ameshaambiwa yanahamasisha yasiyokubalika kwenye jamii. Wimbo huo licha ya kufungiwa na BASATA bado unatumiwa na baadhi ya watu akiwemo Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri, Tulia Ackson, ambae aliuimba na kucheza wakati wakishangilia ushindi wao wa mpira wa wabunge wa Afrika Mashariki.

WASAFI wanahitaji walezi bora zaidi, RC wa Dar Paul Makonda ambae hujinasibu kumshauri Diamond, hatoshi. Nchi imetangazwa juzi kuwekewa maazimio makali na dunia, Waziri wa Fedha katoa tamko kwamba hali ni mbaya kutokana na hayo hayo "mambo ya Amber Rutty." Mtu mwenye busara ungefunika kombe mwanaharamu apite, lakini Makonda kaenda kwenye mic kaongelea tena "mambo ya Amber Rutty." Usiku wake Diamond kapanda jukwaani kaimba tena "mambo ya Amber Rutty" yanaleta "Mwanza Nyegezi."

Bado tatizo la Diamond na waambata wake ni upeo.

Basata wamjadili Diamond kuimba wimbo uliofungiwa
 
Wanajuana hao usiumie kichwa

Diamond huwa anapewa bendera ya nchi na waziri wa utamaduni uwanja wa ndege wa Julius Nyerere kwenda kutuwakilisha. Chochote anachofanya kwa jina letu kinatuhusu!

Hawezi kuwa balozi wa nchi wa "mambo ya Amber Rutty" na ushoga halafu tukasema hayatuhusu.
 
Huyu diamond mwendawazimu hakukuwa na ulazima wa kupiga hiyo nyimbo , wacha wamtie adabu
 
Kwenye daladala (Hiace) za mwanza huu wimbo unapigwa hadi kero.
 
Huu wimbo hauna tatizo lolote. Basata walijichanganya tu
 
Hii nchi hii, ndio maana timu yetu ya Taifa inafungwafungwa hata na viwete.
 
Ukiwa na Bashite uko juu ya sheria, Bashite ni babayetu asiyeshindwa kamwe
 
Umelewa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…