Biashara inapokuwa kubwa, makampuni huwa yanaanzisha kitengo kinaitwa compliance department na huajiri wataalam wa kuhakikisha biashara haibughudhiwi bugudhiwi na serikali kwa kuvunja vunja visheria vidogo vidogo na vikubwa.
Diamond jana, Desemba 15, akiwa Mwanza kaimba tena "mambo ya Amber Rutty." Mkuu wa BASATA katoa tamko la dharura kwamba ameyasikia, yuko njiani Arusha atarudi makao mkuu kumshushia rungu zito kwa sababu Diamond amedharau baraza, wizara na serikali yote kwa kuimba mambo ambayo ameshaambiwa yanahamasisha yasiyokubalika kwenye jamii. Wimbo huo licha ya kufungiwa na BASATA bado unatumiwa na baadhi ya watu akiwemo Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri, Tulia Ackson, ambae aliuimba na kucheza wakati wakishangilia ushindi wao wa mpira wa wabunge wa Afrika Mashariki.
WASAFI wanahitaji walezi bora zaidi, RC wa Dar Paul Makonda ambae hujinasibu kumshauri Diamond, hatoshi. Nchi imetangazwa juzi kuwekewa maazimio makali na dunia, Waziri wa Fedha katoa tamko kwamba hali ni mbaya kutokana na hayo hayo "mambo ya Amber Rutty." Mtu mwenye busara ungefunika kombe mwanaharamu apite, lakini Makonda kaenda kwenye mic kaongelea tena "mambo ya Amber Rutty." Usiku wake Diamond kapanda jukwaani kaimba tena "mambo ya Amber Rutty" yanaleta "Mwanza Nyegezi."
Bado tatizo la Diamond na waambata wake ni upeo.
Basata wamjadili Diamond kuimba wimbo uliofungiwa