Video: DIAMOND aionyeshea serikali kidole cha kati, aimba tena NYEGEZI

Video: DIAMOND aionyeshea serikali kidole cha kati, aimba tena NYEGEZI




Biashara inapokuwa kubwa, makampuni huwa yanaanzisha kitengo kinaitwa compliance department na huajiri wataalam wa kuhakikisha biashara haibughudhiwi bugudhiwi na serikali kwa kuvunja vunja visheria vidogo vidogo na vikubwa.

Diamond jana, Desemba 15, akiwa Mwanza kaimba tena "mambo ya Amber Rutty." Mkuu wa BASATA katoa tamko la dharura kwamba ameyasikia, yuko njiani Arusha atarudi makao mkuu kumshushia rungu zito kwa sababu Diamond amedharau baraza, wizara na serikali yote kwa kuimba mambo ambayo ameshaambiwa yanahamasisha yasiyokubalika kwenye jamii. Wimbo huo licha ya kufungiwa na BASATA bado unatumiwa na baadhi ya watu akiwemo Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri, Tulia Ackson, ambae aliuimba na kucheza wakati wakishangilia ushindi wao wa mpira wa wabunge wa Afrika Mashariki.

WASAFI wanahitaji walezi bora zaidi, RC wa Dar Paul Makonda ambae hujinasibu kumshauri Diamond, hatoshi. Nchi imetangazwa juzi kuwekewa maazimio makali na dunia, Waziri wa Fedha katoa tamko kwamba hali ni mbaya kutokana na hayo hayo "mambo ya Amber Rutty." Mtu mwenye busara ungefunika kombe mwanaharamu apite, lakini Makonda kaenda kwenye mic kaongelea tena "mambo ya Amber Rutty." Usiku wake Diamond kapanda jukwaani kaimba tena "mambo ya Amber Rutty" yanaleta "Mwanza Nyegezi."

Bado tatizo la Diamond na waambata wake ni upeo.

Basata wamjadili Diamond kuimba wimbo uliofungiwa


mi cjaskia diamond akiuimba ila mashabiki
 
Curve inaanaza kutaka ku-bend down wards.
Diamond mashairi yamemuishia anaanza kutafuta jina kwa matusi
 
Curve inaanaza kutaka ku-bend down wards.
Diamond mashairi yamemuishia anaanza kutafuta jina kwa matusi
Safari yake inaelekea ukingoni, anaona ufahari kutoa nyimbo kila kukicha pasipo kuangalia ubora wa nyimbo hizo
 
Diamond huwa anapewa bendera ya nchi na waziri wa utamaduni uwanja wa ndege wa Julius Nyerere kwenda kutuwakilisha. Chochote anachofanya kwa jina letu kinatuhusu!

Hawezi kuwa balozi wa nchi wa "mambo ya Amber Rutty" na ushoga halafu tukasema hayatuhusu.
Kwani kibaya alichokiimba ni nini alichosema " Ila naogopa central michezo ya amber ruty" tatizo hapo liko wapi au tatizo ni hiyo mizee ya basata
 
Kwani kibaya alichokiimba ni nini alichosema " Ila naogopa central michezo ya amber ruty" tatizo hapo liko wapi au tatizo ni hiyo mizee ya basata
Hakika kabisa ,ameonyesha uoga ,kwahiyo hapo amewataka watu kuogopa hili jambo mtaenda jela
 
Back
Top Bottom