Unaposema Magufuli aliupaisha huo ukatili maana yake unakiri ulikuwepo kabla.
Kumbe basi, kosa sio la Magufuli peke yake, hata wapinzani nao wana kosa kwa kushindwa kuulaani huo ukatili ulipotokea mwanzo kwa nguvu ile ile waliyotumia kuulaani wakati wa Magufuli.
Masuala mengine uliyoandika hapo ni tabia binafsi za watu, kwasababu hata kama Ulimboka alitekwa akapigwa, tayari aliumizwa, kutokusemwa vibaya baada ya kupigwa, hakuondoi ukweli kwamba alipigwa na kuumizwa.
..NDIO NDIO NDIO.
..Ninakiri ukatili umekuwepo ktk tawala zote hapa Tanzania.
..Hoja yangu ni kwamba utawala wa Magufuli ulikuwa katili kuliko utawala wa Muingereza, Nyerere, Mwinyi, Mkapa, na Kikwete.
..Hebu tufanye rejea kidogo ktk TAKWIMU na historia.
..Muingereza aliendesha uchaguzi hapa Tanganyika. Je, ulisikia mgombea hata mmoja wa chama cha Tanu kuenguliwa au kudhalilishwa?
..Sasa rudi kati ya 2016 na 2020 Tume ya uchaguzi wa Magufuli iliengua wagombea wangapi wa upinzani. Hesabu zangu zinaniambia ni maelfu.
..Tuje kwenye udhalilishaji, makesi, na vipigo dhidi ya viongozi na wanachama wa upinzani.
..Ukisoma historia ya Tanu kuna kesi kubwa ya Mwalimu, Makange, na Baghdele. Pia kuna kesi ya mgomo wa mabasi kama sikosei. Hazizidi kesi 10.
..Taarifa za hivi karibuni zinasema serikali ya Magufuli iliwabambikia kesi viongozi na wanachama 400++ wa Chadema.
..Je, uliwahi kusikia Nyerere amelazwa mahabusu, amedhalilishwa, au amepigwa na kujeruhiwa na askari wa Mkoloni / Muingereza?
..Hapa naomba nikukumbushe udhalilishaji waliofanyiwa viongozi wa Chadema walipofungwa kwa kesi ya uongo ya maandamano ya uchaguzi mdogo Kinondoni.
..Viongozi wale, wajumbe wa kamati kuu walinyolewa nywele. Walisachiwa wakiwa uchi wa mnyama. Utawala wa Magufuli ulifanya hayo.
..Je, umewahi kusikia Nyerere kanyolewa nywele na askari magereza wa Mkoloni? Umewahi kusikia amedhalilishwa na kusachiwa uchi wa mnyama?
..Nilitegemea Magufuli walau awe na afadhali kuliko Wakoloni, but his regime was more abusive and brutal na nimekupa ushahidi hapo juu.
..Sasa unakuja kwa mwanazuoni Bashiru. Je, hakuyaona hayo? Kwanini hakuyapinga na kuyakemea?
...Natofautiana na madai yako kwamba wapinzani hawakupinga maovu yaliyofanywa na tawala zilizomtangulia Magufuli.