Uchaguzi 2020 VIDEO: Dkt. Magufuli arejea Makao Makuu ya nchi Dodoma, aserebuka wimbo wa Zuchu mbele ya wananchi

Uchaguzi 2020 VIDEO: Dkt. Magufuli arejea Makao Makuu ya nchi Dodoma, aserebuka wimbo wa Zuchu mbele ya wananchi

Baada ya kuanza kampeni za kuwania Urais katikati ya kitovu cha nchi na kwenda mikoa mbalimbali, leo mgombea urais kwa tiketi ya chama cha mapinduzi amerejea mjini Dodoma na kulakiwa na wananchi mbalimbali wa mkoa.

Katika furaha isiyo kifani, Dkt Magufuli amecheza wimbo wa 'Tanzania ya sasa' uliombwa na msanii Zuchu ukipongeza juhudi zake alizozifanya kama Rais na chama chake cha Mapinduzi kuibadilisha Tanzania.

Amefanya mengi makubwa na atashinda ila angepata msaada wa kuweza kukubali hata mapungufu kiasi na kuahidi kuyafanyia kazi.Masula ya uhuru wa watu,kesi za kubambikia,muingiliano wa mihili.Haya angekubali tu kuwa mapungufu na yupo tayari kuyafanyia kazi.
Huu ni wakai wa kuwa humble na kukubali makosa ili atimize alichodhamiria katika maika mingine mitano.
 
Wewe ni wale wanafikiri ngege ni kama mapambo. Hawaoni faida kutokana vibaraka wa mabeberu kuwapotosha. Wanajidai kudai maji baada ya kupiga hela kwa dili zilizojaa ufisadi wa kila aina. Roho zinauma baada ya kutumbuliwa wezi serikalini na fedha kuelekezwa kwenye miradi yenye faida kwa umma.

Tueleze faida za ndege kwa wanaichi wa Tanzania wasio na huduma nzuri ya maji na afya. Twende tu taratibu . Tusitukanane wala kuvunjiana heshima
 
Wewe ni wale wanafikiri ngege ni kama mapambo. Hawaoni faida kutokana vibaraka wa mabeberu kuwapotosha. Wanajidai kudai maji baada ya kupiga hela kwa dili zilizojaa ufisadi wa kila aina. Roho zinauma baada ya kutumbuliwa wezi serikalini na fedha kuelekezwa kwenye miradi yenye faida kwa umma.
2020 OYEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEE
 
Nimekakuta.
Screenshot_20200923-103547.jpg
 
Dah nilikuwa dodoma mjini na gari tulisimamishwa karibia lisaa lizima tokea saa 7 mchana Hadi saa 8 kupisha msafara wake kusema kweli sio fair mmnaoratibu hii misafara.

Embu tumieni logic sio vizurii kuwasimamisha watu muda mrefu (lisaa lizima) kisa kiongozi anataka kupita dalalala nyingi niliona zimepata hasara manake abiria wengi walikuwa wanashuka wanapanda pikipiki kuwahi kwenye shughuli zao kusema ukweli wananchi waliudhika sana.

Mtu anaomba kura akipitishwa akiwa anapita barabarani mnasimamishwa lisaa lizima ile apite yeye na msafara wake wa zaidi ya magari 50 pamoja na zahanati inayotembea halafuanajinasibu eti mimi mtumishi wenu

Angekuwa mtumishi kweli asingethubutu kuwasimamisha wananchi (mabosi) barabarani ili apite yeye
Maswali yaleyale ya yule movu rusfeli; Kama kweli ww ni mwana wa Mungu Basi Fanya hivi au vile...!aJitathiminu ndugu!
 
Umesema kweli ,ila kwa sasa Tanzania ilikuwa hahitaji ndege ,huduma za maji na afya bado ni changamoto ,, je hizo ndege mwanaichi wa Mpanda anafaidikaje nayo!! Bila kupepesa macho Serekali yetu ingefanya vitu vyenye umuhimu kwanza kama Barabara ,maji ,afya etc,, ndo ije kwenye mandege hayo .
Kuna umbumbu mwingine hata unashindwa kujua uanzie wapi kumpa SoMo maana siyo kwa upoyoyo wa kiwango Airbus!
 
Hoja hamna, naona picha zaonesha kampeni imemmaliza mwili mgombea wa CCM, John Magufuli amepungua sana pamoja ya kuwa ni rais lakini haisaidii kweli kampeni hii ya 2020 ni ngumu.

Vipi hiki chama kongwe kukosa sera za kuwaambia wananchi na kuishi kupiga Muziki huko kote alipopita mgombea John Magufuli wa CCM.
Hivi ni kweli hujaona sera!?, Wapi ulikoona sera
 
Kuna umbumbu mwingine hata unashindwa kujua uanzie wapi kumpa SoMo maana siyo kwa upoyoyo wa kiwango Airbus!

Tunakwenda nayo taratibu hivo hivo ,, Inchi kuwa na shirika lake imara la usafirshaji wa anga ni jambo zuri ,kwa hali ya Tanzania ya sasa ndege zilikuwa bado sio muhimu kwetu,, tungeboresha kwanza huduma za afya ,elimu ,barabara etc . Je ni sahihi baba kujenga gorofa huku watoto wanapata kwashakoo ,! Haraka haraka utajijibu hapana. Kwahiyo Jiwe anachokifanya sio sahihi.

Pia kujenga uwanja wa ndege Chato wa kimataifa,sio sahihi kabisa , .Japikuwa chato ni Tanzania , why isiwe mwanza kwenye muingiliano mkubwa wa watu na uhitaji mkubwa !! . Tunapaswa kufanya mambo kwa priorities!!
 
Kwa Nini KIA wakati Kuna Arusha airport?
 
Duniani Mgombea yoyote wa siasa anapowania kiti cha kuchaguliwa na wananchi, lazima awe myenyekevu. Sio magufuli pekee. Hata lissu akichaguliwa atakuwa mbogo na hataonekana kirahisi, tusidanganyane.
Kila mahali kuna Bango la Meko. Tunakaribia kumaliza Kampeni na bado sijaona bango hata moja la Tundu Lissu.

Swali: anawezaje kupata Nyomi kwenye mikutano ya hadhara bila ya matangazo? System wangetafakari hili swali sana maana jibu lake linaweza kuwaelimisha

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tunakwenda nayo taratibu hivo hivo ,, Inchi kuwa na shirika lake imara la usafirshaji wa anga ni jambo zuri ,kwa hali ya Tanzania ya sasa ndege zilikuwa bado sio muhimu kwetu,, tungeboresha kwanza huduma za afya ,elimu ,barabara etc . Je ni sahihi baba kujenga gorofa huku watoto wanapata kwashakoo ,! Haraka haraka utajijibu hapana. Kwahiyo Jiwe anachokifanya sio sahihi.

Pia kujenga uwanja wa ndege Chato wa kimataifa,sio sahihi kabisa , .Japikuwa chato ni Tanzania , why isiwe mwanza kwenye muingiliano mkubwa wa watu na uhitaji mkubwa !! . Tunapaswa kufanya mambo kwa priorities!!
Mifano uliyotumia Haina uhusiano na hayo matukufu ya Magufuli! Hapa Kuna maamuzi ya kuipanda ama kukaanga na kula mbegu! Magu kaamua kuzipanda, wenye njaa wanamlalamikia Leo Ila kesho watacheka na kumshukuru!
 
Hii mada imekuzidi upeo ,kaa pembeni.
 
Back
Top Bottom