..kila mtu anajua kilichotokea.
..nadhani hakuna haja ya kubishana kuhusu nini kilitokea.
..we should come together as a nation kuangalia namna bora ya kuwafariji walioumizwa.
..ningependa wachangiaji wanaotukanana ktk mjadala huu wavae viatu vya wazazi wa Ben Saanane.
..tujiulize wazazi wa Ben Saanane wanaamkaje, wanashindaje, na wanalalaje?
..Kabla ya ku-post tuwafikirie mke, watoto, na wazazi wa Azory Gwanda. Hivi tumewaona jinsi walivyo masikini? Na Azory ndio alikuwa tegemeo lao.
..Tukirudi kwa Fatma Karume, ofisi yake imepigwa bomu. Je, kilichotokea ni uungwana? Je, ni halali? Je, amepata haki yake?
..Je, Fatma ame-react kinyume na matarajio? Kwanini tunaona ajabu Fatma Karume kulalamika? Nini kifanyike ili Fatma Karume na wengine waliofikwa na majanga wasilalamike?
..Again, natamani Watanzania tuwe kitu kimoja na kushinikiza HAKI itendeke kwa wote walioumizwa.