Humu kuna watu hawataki yasemwe kwa uwazi mabaya aliyofanya Magufuli..
Kila binadamu ana udhaifu fulani na ndio maana kila muda kwenye nyumba za ibada tunakumbushwa kuomba toba.
Magufuli kama binadamu aliyepita inabidi asemwe kusudi iwe fundisho kwa vizazi vijavyo kwa namna ya kupata viongozi wenye busara na ngozi nene ( kuhimili changamoto za kiuongozi)
Magufuli hakuweza kuhimili changamoto na hivyo kujikuta anaumiza watu kwakuwa alikuwa na cheo kikubwa kilichompa kiburi.
Lazima Magufuli asemwe kwakuwa hakufuata sheria.. Alipenda sifa binafsi na kujiona kwamba yeye ndiye mwenyewe yupo sahihi.
Lazima asemwe ili iwe fundisho kwa taifa hasa kupata kiongozi mwenye utimamu wa akili katika kuongoza watu na taasisi zake kwa kufuata sheria.. Na kuondoa UMIMI kwa kila jambo mpaka taifa kujikuta amevuruga kila kitu.. Kuanzia ajira, biashara ( kaharibu sekta binafsi Sana), mahusiano ya kimataifa, siasa za manunuzi, siasa za risasi, siasa za zidumu fikra za mwenyekiti..
Alikwenda kufanya Mahakama ziwe hovyo sana hasa pale Serikali ikiwa inalalamikiwa..
Magufuli hakufaa kuwa Rais, alijaa roho ya visasi sana