Video: Fatma Karume Kwenye Mhadhara wa Kimataifa Asimulia Unyama wa "Kinyago Tulichokichonga Wenyewe"

Video: Fatma Karume Kwenye Mhadhara wa Kimataifa Asimulia Unyama wa "Kinyago Tulichokichonga Wenyewe"

Warumi 13:1-3.
1.Kila mtu mtu na atii mamlaka iliyo kuu,kwa maana hakuna mamlaka isiyotoka kwa Mungu,na ile iliyopo umeamriwa na Mungu.
2.Hivyo amwasiye mwenye mamlaka hushindana na agizo la Mungu,nao washindanao watajipatia hukumu.
3.Kwa maana watawalao hawatishi watu kwa sababu ya matendo mema,bali kwa sababu ya matendo mabaya.Basi,wataka usimuogope mwenye mamlaka?Fanya mema nawe utapata sifa kwake...
Tofasiri yake unaijua? Herode alikuwa ni mwenye mamlaka, lakini alipingwa na Yohana mbatizaji kwa madhambi yake, Yohana akachinjwa. Jitahidini kujua ya kutii mamlaka vinginevyo mtakuwa wapotoshaji tu. Wale vijana watatu wacha Mungu, Daniel, Meshack na Abdinego walimgomea Mfalme Nebkadneza wakatupwa kwenye tanuru la moto, Swali: Nebkadneza hakuwa na mamlaka kuu?
 
Yule nduli aliepita lazima asemwe kwa nguvu zote. Hitler, Bokassa, Amini, Mobuttu wanasemwa kwa mabaya yao,

Sasa iweje Magufuli akisemwa iwe nongwa?!
 
Kwani na wewe umekatazwa kuzunguka duniani kueleza ukatili wa babu yake dhidi ya Wazanzibari?

Kwani Fatma Karume ndiye aliyesababisha babu yake afanyie ukatili Wazanzibari?

Kwani ikiwa babu yake kafanyia ukatili Wazanzibari, hilo linaondoa ukweli atakaousema kuhusu Magufuli?
Hoja nzito sana hizi.
Safi sana
 
Anatakaje?

Yupo oslo kutafuta sympathy?

Ama bado sijaelewa motive yake?

Tumshtaki Magufuli huko kaburini ama?
 
ukweli maana yake nini mkuu???

isiwe ukweli ni tuhuma zozote zinazomkabili usiyempenda.
hapa ndio maama mwanaharakati uchwara anapokabwa kwamba harakati haziangalii nani yako kafanya,unatakiwa ufumue kote kote.

huu utoto wa kuwaambia watu wakausemee na wao wakati tunapishana vipaumbele,hulka,mifumo ya maisha na malengo ni dalili ya ushabiki.
Nakwambia hivi, two wrongs do not make a right.

Yani hata kama Fatma kawa selective kumsema Magufuli, kama tuhuma zake dhidi ya Magufuli ni za kweli, zitabaki kuwa kweli tu.

Sasa hapa suala ni, je, tuhuma za Fatma dhidi ya Magufuli ni za kweli?

Huko kwa Karume hata mimi nayajua maovu aliyoyatenda.

Na wala sijasema kwamba Fatma is infallible. She is from a political family after all.

Lakini, Karume kufanya mabaya hakumaanishi kwamba Magufuli hakufanya mabaya.

Kwa nini mnaleta distraction ya Karume kama vile inaondoa mabaya ya Magufuli?

Sasa wewe unayajua mabaya ya Karume, na unaona ni muhimu yasemwe leo, halafu kazi ya kuyasema mabaya ya Karume unamuachia mjukuu wake?

Unaona habari hiyo ina mantiki?
 
Anatakaje?

Yupo oslo kutafuta sympathy?

Ama bado sijaelewa motive yake?

Tumshtaki Magufuli huko kaburini ama?

..Magufuli hata angekuwa hai asingeweza kushtakiwa kwasababu Maraisi wana kinga ya kutoshtakiwa.

..Lakini kuna wahusika waliopokea na kutekeleza maagizo ya kuteka, kutesa, na kuua. Wahusika hao wanatakiwa kushtakiwa.
 
Fatuma kenge tu utawala wa babu na baba yake walikufa wengi sana
 
Humu kuna watu hawataki yasemwe kwa uwazi mabaya aliyofanya Magufuli..
Kila binadamu ana udhaifu fulani na ndio maana kila muda kwenye nyumba za ibada tunakumbushwa kuomba toba.

Magufuli kama binadamu aliyepita inabidi asemwe kusudi iwe fundisho kwa vizazi vijavyo kwa namna ya kupata viongozi wenye busara na ngozi nene ( kuhimili changamoto za kiuongozi)

Magufuli hakuweza kuhimili changamoto na hivyo kujikuta anaumiza watu kwakuwa alikuwa na cheo kikubwa kilichompa kiburi.

Lazima Magufuli asemwe kwakuwa hakufuata sheria.. Alipenda sifa binafsi na kujiona kwamba yeye ndiye mwenyewe yupo sahihi.

Lazima asemwe ili iwe fundisho kwa taifa hasa kupata kiongozi mwenye utimamu wa akili katika kuongoza watu na taasisi zake kwa kufuata sheria.. Na kuondoa UMIMI kwa kila jambo mpaka taifa kujikuta amevuruga kila kitu.. Kuanzia ajira, biashara ( kaharibu sekta binafsi Sana), mahusiano ya kimataifa, siasa za manunuzi, siasa za risasi, siasa za zidumu fikra za mwenyekiti..
Alikwenda kufanya Mahakama ziwe hovyo sana hasa pale Serikali ikiwa inalalamikiwa..

Magufuli hakufaa kuwa Rais, alijaa roho ya visasi sana
 
Serikali kwa sasa ina Rais mwingine ambaye anafanya jitihada za maridhiano. Naamini kama kuna ushahidi dhidi ya makosa ya mtangulizi wake, kama hayo yaliyotajwa, ni wakati mwafaka kuyawasilisha kwenye vyombo vya haki, ndani na nje ya nchi. Kuendelea kutuhumu, kama Wakili msomi, Fatma, inafikirisha na kumwondoa kwenye ustaarabu. AIBU.
Kumfikisha marehemu kwenye vyombo vya haki?
 
Warumi 13:1-3.
1.Kila mtu mtu na atii mamlaka iliyo kuu,kwa maana hakuna mamlaka isiyotoka kwa Mungu,na ile iliyopo umeamriwa na Mungu.

2.Hivyo amwasiye mwenye mamlaka hushindana na agizo la Mungu,nao washindanao watajipatia hukumu.

3.Kwa maana watawalao hawatishi watu kwa sababu ya matendo mema,bali kwa sababu ya matendo mabaya.

Basi, wataka usimuogope mwenye mamlaka?Fanya mema nawe utapata sifa kwake...
Ni mamlaka zilizopatikana kihalali pekee la sivyo hata waliojitwalia mamlaka kwa kutofuata utaratibu nao watajiona wana haki.
 
Huko Philippines kwenye Uchaguzi ulioisha Ferdinand Romualdez Marcos, ameshinda Uchaguzi wa Urais licha ya kuwa baba yake Mzazi Ferdinand Marcos alikuwa DIKTETA na alipinduliwa kwa nguvu ya umma kwenye miaka ya 1980s


Kamwe matendo ya Baba au Babu hayamhusu mwana au mjukuu
Papai halizai embe.
 
I am one among the annoyed ones! Why would she speak the truth behind Magufuli's back?

Why did Fatma hesitate to face Magufuli and tell him that his regime had dragged the country back to the dark ages?

She said she was brought up in the democratic home why did she fear Magufuli?

Why does she speak the

Anazani watanzania ndyo watamuelewa?? aliye tu na uhakika hata akigombea leo na huyo anaemponda wtu watachagua kivuli kuliko yy
Sikusikia anatafuta kura.
 
Clip ya Dak 2:47 akiwa Oslo Forum anasimulia namna "Kinyago Tulichokichonga Wenyewe" namna kilivyo piga bomu ofisi yake ya UWAKILI na kumjeruhi Tundu Lissu kwa risasi 16.

Hatimaye Kinyago chenyewe kilinyauka mnamo 17/ 03/ 21.

View attachment 2241890
Clip ya Dak 2:47 akiwa Oslo Forum anasimulia namna "Kinyago Tulichokichonga Wenyewe" namna kilivyo piga bomu ofisi yake ya UWAKILI na kumjeruhi Tundu Lissu kwa risasi 16.

Hatimaye Kinyago chenyewe kilinyauka mnamo 17/ 03/ 21.

View attachment 2241890
She is most intelligent and courageous person in history of our country. No doubt about her. Fatma you are the best!
 
Back
Top Bottom