Video: Fatma Karume Kwenye Mhadhara wa Kimataifa Asimulia Unyama wa "Kinyago Tulichokichonga Wenyewe"

Video: Fatma Karume Kwenye Mhadhara wa Kimataifa Asimulia Unyama wa "Kinyago Tulichokichonga Wenyewe"

Clip ya Dak 2:47 akiwa Oslo Forum anasimulia namna "Kinyago Tulichokichonga Wenyewe" namna kilivyo piga bomu ofisi yake ya UWAKILI na kumjeruhi Tundu Lissu kwa risasi 16. Hatimaye Kinyago chenyewe kilinyauka mnamo 17/ 03/ 21
View attachment 2241890
Serikali kwa sasa ina Rais mwingine ambaye anafanya jitihada za maridhiano. Naamini kama kuna ushahidi dhidi ya makosa ya mtangulizi wake, kama hayo yaliyotajwa, ni wakati mwafaka kuyawasilisha kwenye vyombo vya haki, ndani na nje ya nchi. Kuendelea kutuhumu, kama Wakili msomi, Fatma, inafikirisha na kumwondoa kwenye ustaarabu. AIBU.
 
Ngoja waje
JamiiForums-266676641.jpg
 
Ni kweli lkn ukatiri wa JPM lazima usemwe.
Na ninaamini kwa sasa yuko jehanamu akichomwa barabara.
Tena leo kadudu kake ndio kanaunguzwa
Mh! Kuna namna sio bure hadi utaje dudu katika mwili wote.

Huyu Magufuli usikute aliwafanya watu vibaya kuliko haya yenye kusemwa hadharani.
 
Serikali kwa sasa ina Rais mwingine ambaye anafanya jitihada za maridhiano. Naamini kama kuna ushahidi dhidi ya makosa ya mtangulizi wake, kama hayo yaliyotajwa, ni wakati mwafaka kuyawasilisha kwenye vyombo vya haki, ndani na nje ya nchi. Kuendelea kutuhumu, kama Wakili msomi, Fatma, inafikirisha na kumwondoa kwenye ustaarabu. AIBU.
Kuongea mambo yaliyokukuta hakuondoi ustaarabu wako na wala haupati aibu.
 
Warumi 13:1-3.
1.Kila mtu mtu na atii mamlaka iliyo kuu,kwa maana hakuna mamlaka isiyotoka kwa Mungu,na ile iliyopo umeamriwa na Mungu.
2.Hivyo amwasiye mwenye mamlaka hushindana na agizo la Mungu,nao washindanao watajipatia hukumu.
3.Kwa maana watawalao hawatishi watu kwa sababu ya matendo mema,bali kwa sababu ya matendo mabaya.Basi,wataka usimuogope mwenye mamlaka?Fanya mema nawe utapata sifa kwake...
Hiyo Biblia mnaitumia vibaya. Na siku zote mnajificha kwenye huo mstari wa kwamba tutii Mamlaka kwa vile zinatoka kwa Mungu. Mbona Mungu mwenyewe alimtuma Musa kuwakomboa wana wa Israel toka kwa Farao?

Mungu anasingiziwa matendo machafu ya binadamu. Siamini kama Mamlaka ya Adolf Hitler ilitoka kwa Mungu. Vivyo hivyo siamini kuwa Mamlaka ya Magufuli ya uwizi wa kura za Oktoba 2020 ilitoka kwa Mungu. Na kuthibitisha hilo Mungu kachukua roho yake ndani ya siku 120 baada ya kuiba kura
 
Not sexism nor misogyny, but does she talk to her husband and their kids in the same hatred language?
Nenda kamuulize mumewe swali hilo kama hujakula vitasa! Usiende nje ya mada hata kama wewe ni worshiper wa Mwendazake
 
Inategemea hasa ukiwa haujawahi kuangukiwa na kinyago.
Nimezungumzia maana ya msemo wa kinyago, angeweza kutumia neno dikteta au lengine ila msemo wa kinyago ulichokichongo mwenyewe una maana ya kitu ambacho hauwezi kukiogopa, sasa Jiwe sio tu kwamba alikuwa anatisha bali alikuwa anadhuru kabisa sasa unamwiitaje kuwa ni kinyago ulichokichonga?
 
Mara nyingi ni ngum sana kujitenga na makosa aliyofanya mzazi wako especial katika field hii ya siasa,ndo maana hata Mungu alikuwa anatoa laana ya vizazi na vizazi wakati kosa alifanya mmoja.Fatma akitaka baba ake apumzishwe aache kusema baba wa wenzake.
Huko Philippines kwenye Uchaguzi ulioisha Ferdinand Romualdez Marcos, ameshinda Uchaguzi wa Urais licha ya kuwa baba yake Mzazi Ferdinand Marcos alikuwa DIKTETA na alipinduliwa kwa nguvu ya umma kwenye miaka ya 1980s

Kamwe matendo ya Baba au Babu hayamhusu mwana au mjukuu
 
Nimezungumzia maana ya msemo wa kinyago, angeweza kutumia neno dikteta au lengine ila msemo wa kinyago ulichokichongo mwenyewe una maana ya kitu ambacho hauwezi kukiogopa, sasa Jiwe sio tu kwamba alikuwa anatisha bali alikuwa anadhuru kabisa sasa unamwiitaje kuwa ni kinyago ulichokichonga?
Ama kweli umepotea njia. Huu ni msemo tu na siyo kwamba anasema kuwa Jiwe hakuwa anatishia watu. Magufuli alikuwa mtu katili na angeweza kuagiza mtu afanyiwe jambo lolote ili tu aonekane yeye ni zaidi. Sasa huu msemo una maana kuwa pamoja na hayo yote lakini alikuwa pale kwa sababu yetu inabidi kila mwananchi kutokuogopa kusema anapofanya mabaya.
 
Back
Top Bottom