Video: Fatma Karume Kwenye Mhadhara wa Kimataifa Asimulia Unyama wa "Kinyago Tulichokichonga Wenyewe"

Video: Fatma Karume Kwenye Mhadhara wa Kimataifa Asimulia Unyama wa "Kinyago Tulichokichonga Wenyewe"

Hiyo Biblia mnaitumia vibaya. Na siku zote mnajificha kwenye huo mstari wa kwamba tutii Mamlaka kwa vile zinatoka kwa Mungu. Mbona Mungu mwenyewe alimtuma Musa kuwakomboa wana wa Israel toka kwa Farao?

Mungu anasingiziwa matendo machafu ya binadamu. Siamini kama Mamlaka ya Adolf Hitler ilitoka kwa Mungu. Vivyo hivyo siamini kuwa Mamlaka ya Magufuli ya uwizi wa kura za Oktoba 2020 ilitoka kwa Mungu. Na kuthibitisha hilo Mungu kachukua roho yake ndani ya siku 120 baada ya kuiba kura
Punguza povu mkuu,sijakwambia ufuate nilichopost wala sijaongeza neno langu hapo,hayo ni maandiko matakatifu ndio yameongea,so you just take or leave it...
 
Ama kweli umepotea njia. Huu ni msemo tu na siyo kwamba anasema kuwa Jiwe hakuwa anatishia watu. Magufuli alikuwa mtu katili na angeweza kuagiza mtu afanyiwe jambo lolote ili tu aonekane yeye ni zaidi. Sasa huu msemo una maana kuwa pamoja na hayo yote lakini alikuwa pale kwa sababu yetu inabidi kila mwananchi kutokuogopa kusema anapofanya mabaya.
Kila msemo una maana na matumizi yake, ccm wenyewe naona ndio wangefaa kuutumia huo msemo.
 
Serikali kwa sasa ina Rais mwingine ambaye anafanya jitihada za maridhiano. Naamini kama kuna ushahidi dhidi ya makosa ya mtangulizi wake, kama hayo yaliyotajwa, ni wakati mwafaka kuyawasilisha kwenye vyombo vya haki, ndani na nje ya nchi. Kuendelea kutuhumu, kama Wakili msomi, Fatma, inafikirisha na kumwondoa kwenye ustaarabu. AIBU.
Watanzania wengine sijui akili mnazipeleka wapi. Nitakuambia ofisi ya Fatma ilipokuwa halafu uniambie ni nani anaweza kuingia pale kupiga bomu kama siyo mtu aliyetumwa na mtu mwenye nguvu kuliko wote Tanzania.

Ofisi ilikuwa opposite Almuntanzir School, Barbara ya United Nation. Ni mita 200 hadi kituo nyeti cha Saleander Bridge Police, mita 200 pembeni ya makao makuu ya TAKUKURU na Mita 500 hadi Ngome ambayo ni makao makuu ya JWTZ.

Nani anaweza kufanya uhalifu kama huo kama hakutumwa na Magufuli mwenyewe?

Subiri hiyo Time iundwe tutapeleka ushahidi. Mbona hata voice clip ya kum shoot Tundu Lissu IPO na Magufuli mwenyewe kaongea!!
 
Japo Lissu mlemavu lakini kashuhudia mtesi wake akifa. Ndiyo raha yenyewe
Hakuna raha hapo maana hata yeye anajua atakufa pamoja na ulemavu wake ila sio kila mtu atapata ulemavu kama yeye.

Ingekuwa yeye ndio kasababiaha hicho kifo kweli ila sio mtu kafa tu mwenyewe huko na wewe hujawahi hata kumlipizia kofi kisha unsema raha kushuhudia kifo chake tena cha kawaida tu?

Hapo ni sawa na 1-0.
 
Fatma ni Genius ila shida ya Fatma ni moja tu ni mbinafsi sana na hajijui, hivi mama yangu huyu hayakuzi sana ya kwake tu? kupigwa bomu moja tu basi mayowe dunia nzima na imekuwa shida kubwa wakati sisi Chadema tukiongozwa na Miwani Makengeza bin Mbowe bwana wa Mukya na Lipumba na Zana za Kilimo ( ZZK) kila siku twapigwa mabomu, majigumi, majiteke na majirungu na Makonde na maafande mbona hatusemei kwa wazungu?

Mbona shida za wabongo Fatma hazisemi kwa wazungu kama vile m-bara ukienda Zenji kwao wanakuita chogo wanakubagua na kukunyima urojo , mke, chumba cha kupanga na mapembe (wali).wanakula wao tu! Mbona sisi wabara Fei Toto (Zanzibar finest) tumempa jezi yenye namba ya ushindi na kukubali apasiane na Mayele ili wananchi tuteteme?

Mbona Fatma hawaambii wazungu waingilie kuhusu katiba mpya wakati Fatma ni msomi anajua na alisema kuandamana ni kupoteza muda? mbona Fatma hasaidii kuongeza kelele za kudai katiba mpya?

Mbona Fatma hasaidii kupaza sauti kuhusu watoto wasio na uangalizi (abandoned kids) kuzagaa mitaani bongo huku nguo zao zikiwa ziimejaa viraka, wakitaabika na njaa mitaani.

mbona Fatma hawaambii wazungu kuhusu wabongo wengi kulala njaa daily, vijana kuzurura mitaani kumaliza soli za viatu kwa kuuza karanga na mayai na wanunuzi hamna, mbona hasemi dada yake wa Royo Tua kuhusika katika mradi wa kuvunjia maskini vibanda vya bizness baada ya MagufulI kufa na kuwafanya omba omba?

mbona hasemi matajiri kupandisha bei ya wese maradufu na Dada yake kuwakamua tozo kubwa masikini wa bara?

mbona hasemi manesi hawana elimu ya kutosha wanachofanya ni kuchoma watu sindano nyingi wakati ugonjwa mdogo,

mbona hasemi watoto kukaa chini na kushinda na njaa mashuleni kwa kisingizio cha extra classes, mbona Fatma hasemi wazee kulazimisha kufanya kazi maofisini bungeni serikalini huku wakiwa wamechoka vijana wakizurura na bahasha bila ajira, mbona hakemei kukatika umeme kila siku na mabomba kutoa hewa badala ya maji!@ Mbona hamkemei Makamba kutuharibia wizara?

Mwisho wa clip Fatma anasema kuhusu maiti kuokotwa ufukweni na risasi alizopigwa Tindo Less ila nimependa pale amesema alipeleka mahakamani kesi ya kudai tume huru ya uchaguzi, mbona hajamalizia kusema kafikia wapi clip mmeikata? mtoa mada please weka clip yote "mbona kama ishanivutia sana ati" !!

Team gani mmefurahia sana Fatma akimponda sana Magu humu kwenye clip kama dikteta akifananisha na usiku wa giza kweli Magu kile ni chuma hata sasa amekufa ila bado anazungumzwa dunia nzima!!
 
Jiwe hakuwa kinyago, msemo wa kinyago una maana ya kitu ambacho kinatisha tu ila hakina madhara sasa kuna kinyago chenye kupiga bomu na risasi?
Ni figurative language, ni kama mtu anavyosema kinyago nilichokichonga mimi hakiwezi kunitisha, hamaanishi kinyago in literal sense
 
Sijui kama umeelewa.Haiwezekani mzazi wako atende/alitenda kosa au kuvunja sheria halafu weye uende Jela au utumikie adhabu badala yake.Watakaokuhukumu watakuwa vichaa.
Nadhani hatuzungumzii ishu za kimahakama hapa maana kama ni hivyo hata Fatmah hana mamlaka ya kumuhukum Magufuli bila ushahidi au maamuzi ya court of law.
 
Nadhani hatuzungumzii ishu za kimahakama hapa maana kama ni hivyo hata Fatmah hana mamlaka ya kumuhukum Magufuli bila ushahidi au maamuzi ya court of law.
Afadhali yeye kamtuhumu moja kwa moja huyo "kinyago" na hakumtumia mtu mwingine.Hata hivyo,sitarajii ukubaliane na Fatma kwa sababu tu hutaki kukubaliana naye.
 
Hakuna raha hapo maana hata yeye anajua atakufa pamoja na ulemavu wake ila sio kila mtu atapata ulemavu kama yeye.

Ingekuwa yeye ndio kasababiaha hicho kifo kweli ila sio mtu kafa tu mwenyewe huko na wewe hujawahi hata kumlipizia kofi kisha unsema raha kushuhudia kifo chake tena cha kawaida tu?

Hapo ni sawa na 1-0.
Lissu yupo hai, anaweza kuongea, kutembea na kufanya siasa kama kawaida, alizunguka nchi nzima akipiga kampeni bila tatizo lolote.. Jiwe ameshaoza

Kila mtu atakufa ndio, sasa kama ni hivyo kwa nini alitaka kumuua Lissu asisubiri akafa mwenyewe naturally? Maana alijua kuna kitu fulani atakifaidi kwa Lissu kufa mapema sio?
Sasa hicho alichotaka kukipata hakukipata ila Lissu ndio kakipata, yeye kafa mapema, Lissu anaishi
 
Clip ya Dak 2:47 akiwa Oslo Forum anasimulia namna "Kinyago Tulichokichonga Wenyewe" namna kilivyo piga bomu ofisi yake ya UWAKILI na kumjeruhi Tundu Lissu kwa risasi 16. Hatimaye Kinyago chenyewe kilinyauka mnamo 17/ 03/ 21
View attachment 2241890
Umenena vema Shangazi,Kinyago chetu wenyewe kilijipa mamlaka ya kutukosoa kwa umahiri wetu wa kuchonga.
Nakulilia Tanzania ya Tanganyika na Zanzibar, mbona umetutelekeza wanao?
 
Clip ya Dak 2:47 akiwa Oslo Forum anasimulia namna "Kinyago Tulichokichonga Wenyewe" namna kilivyo piga bomu ofisi yake ya UWAKILI na kumjeruhi Tundu Lissu kwa risasi 16. Hatimaye Kinyago chenyewe kilinyauka mnamo 17/ 03/ 21
View attachment 2241890
She is speaking the truth that annoys most of the pro Magufuli's legacy worshipers..

And again, I am very impressed with shangazi's diction and articulation of her English Language..

Her accent is just like of the language owners - the British...
 
Lissu yupo hai, anaweza kuongea, kutembea na kufanya siasa kama kawaida, alizunguka nchi nzima akipiga kampeni bila tatizo lolote.. Jiwe ameshaoza

Kila mtu atakufa ndio, sasa kama ni hivyo kwa nini alitaka kumuua Lissu asisubiri akafa mwenyewe naturally? Maana alijua kuna kitu fulani atakipata kwa Lissu kufa mapema sio?
Sasa hicho alichotaka kukipata hakukipata ila Lissu ndio kakipata, yeye kafa mapema, Lissu anaishi
Ukweli huu wengi wanajaribu kuukwepa na kuukataa kwa hoja za ajabu ajabu sana...

Ila ukweli upo na umesimama tisti kuwa, Hayati Rais John P. Magufuli ndiye aliyeamuru Tundu Lissu kupigwa risasi ama auwawe kwa njia yoyote ile bila sababu yoyote ile..!!

In any case, hakuna sababu yoyote inayoweza ku - justify mtu mwingine kumuua binadamu mwenzake...

Magufuli hakuwa na sababu ya kutoa amri ya kuuwawa mtu huyu...

Inawezekana sababu ikawa;

"...Tundu Lissu alikuwa anamkera sana Rais Magufuli.."

Kama hii (na ofcoz ndivyo ilivyo) ndiyo sababu, basi naweza kusema bila shaka yoyote kuwa, basi huyu alikuwa Rais mjinga, dhaifu na mpumbavu sana...!

Mungu aliyetuumba tunamkosea kila siku. Tuna mkera kila siku. Tunamtukana kila aina aina ya matusi, lakini haamuru tupigwe risasi 37 kila mtu tufe!

Yeye Magufuli alikuwa nani ajichukulie sheria ya Mungu ya kuua mikononi mwake...?

It was a big mistake of his life time na ambalo limegharimu maisha yake, na definitely, alistahili AFE HUYO..!
 
Back
Top Bottom