SI KWELI Video, Haaland akijiogopa baada ya kujiona kwenye kioo

SI KWELI Video, Haaland akijiogopa baada ya kujiona kwenye kioo

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Wakuu hii video ni halisi huyu ni Haaland kweli?

Screenshot 2026-07-01 160404.png
 
Tunachokijua
Kumekuwa na kipande cha video kinachomuonesha mchezaji wa Manchester City na timu ya taifa ya Norway akiwa anakula na kujitizama kwenye kioo na kushtuka.

Ufuatiliaji wa JamiiCheck umejiridhisha kuwa video hiyo imehaririwa sura (Face manipulation) kwa kutumia AI na hivyo anayeonekana kwenye video hakuwa Erling Haaland.

Video halisi ilikuwa ikumuonesha mwanaume wa kichina akiwa kwenye mgawahawa akiwa anakula chakula, tazama hapa.

Huu ni mfano wa namna Teknolojia inaweza kutumika kubadili sura ya mtu na kumuhusisha na tukio ambalo hakuwahi kulifanya hapo awali.
Back
Top Bottom