Wakuu,
Kuna huu mkutano wa Tanzania Personal Secretaries Association (TAPSEA) wa vitengo mbalimbali serikalini unaendelea muda huu na Makamu wa Rais Philip Mpango ndio mgeni rasmi lakini kuna kitu sijaelewa.
Yaani mkutano mzima hawa wazungumzaji wanamsifia na kuimba nyimbo za kumsifu Rais Samia tu as if ni mkutano wa Kamati Kuu ya CCM.
Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
Kulikuwa na haja gani ya kumtaja na kumsifia Rais katika mkutano kama huu? Au hawa wote ni makada wa chama cha mapinduzi?
Na kwenye huu mkutano mgeni rasmi ni Makamu wa Rais, kwanini kuna picha kubwa ya Rais huko nyuma?
Tukisema huu ni mkakati wa kisiasa na kampeni za CCM tutakuwa tunakosea?