SI KWELI Video hii ikimuonesha mwanamke akiendesha pikipiki kwenye barabara ya zege isiyokauka ni halisi

SI KWELI Video hii ikimuonesha mwanamke akiendesha pikipiki kwenye barabara ya zege isiyokauka ni halisi

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Mdau shiriki kuthibitisha Video inayomuonesha mwanamke anayeendesha pikipiki katika barabara inayoendelea kujengwa kwa zege kama ni halisi au imetengenezwa.



1748327775817.png
 
Tunachokijua
Akili Unde (AI) ni seti ya teknolojia zinazoiwezesha kompyuta kutekeleza majukumu mbalimbali ya kina na kwa uwezo mkubwa kadri ya maelekezo ya mtumiaji, ikiwa ni pamoja na uwezo wa kuona, kuelewa na kutafsiri lugha inayozungumzwa na maandishi, kuchanganua data, kutengeneza picha na video na kutoa mapendekezo ya utatuzi wa matatizo mbalimbali.

Aidha teknolojia hii imekuwa muhimu katika kurahisisha ufanisi wa shughuli za kila siku na hii ni pindi tu inapotumika kwa nia iliyo njema, lakini inapotumiwa kwa nia ovu huweza kusababisha madhara makubwa kwa watu, mathalani uwepo wa taarifa potofu unachangiwa pia na teknolojia hii ambayo watu hutumia kutengeneza na kusambaza taarifa zisizo sahihi mfano picha, sauti, na video.

Ipo video iliyochapishwa katika mtandao wa Instagram Video ikimuonesha mwanamke anayeendesha pikipiki katika barabara inayoendelea kujengwa kwa zege imetia shaka kama ni halisi ama ni ya kutengenezwa.


Je, Uhalisia ni Upi?

Kwa kuzingatia mapungufu yaliyobainika katika video hiyo, yanayokinzana na uhalisia, JamiiCheck imejiridhisha kuwa Video hiyo ni ya kutengenezwa kwa haiakisi uhalisia.

Kupotea kwa mkono mmoja wa fundi akiwa ameshikilia kifaa cha kusambazia zege kwa mmoja unaobakia, sehemu ya barabara iliyowekewa zege kutawanyika mithili ya kufanana na maji si kawaida kwani mara baada ya kupita kwa tairi za pikipiki ilipaswa kuonesha alama zake lakini sehemu hizo zinarudi kuwa kawaida bila kuonesha uharibifu. Pia tairi za pikipiki hiyo hazioneshi kuchafuliwa baada ya kupita kwenye zege hilo, kwani zimeendelea kubaki na mng'ao wake wa awali.

Vilevile mwanamke anayeendesha pikipiki kadiri, anavyosogea mbele sura yake inabadilika katika umbo lisilo la kawaida.

Kwa kutumia sehemu ya picha katika video hiyo, kifaa cha kutambua maudhui yaliyotengenezwa kwa akili unde kinabainisha kuwa asilimia 96 imetengenezwa kwa teknolojia hiyo.
screenshot-2025-05-31-155524-png.3352027

​
Back
Top Bottom