Video hii inatosha kutukumbusha utofauti mkubwa kati ya siasa za Marekani na Tanzania

Video hii inatosha kutukumbusha utofauti mkubwa kati ya siasa za Marekani na Tanzania

Keynez

JF-Expert Member
Joined
Feb 12, 2007
Posts
3,809
Reaction score
6,948
Najua wengi mnayafahamu mengi kuhusu tofauti za kimfumo na hata kiutamadumi katika siasa za Tanzania dhidi ya zile za Marekani.

Moja ya jambo ambalo wengi wanaliongelea sana ni uhuru wa vyombo muhimu katika ufanyaji wa kazi na majukumu ya kisiasa.

Huko Marekani, taasisi moja ambayo ufanyaji wake wa kazi umekuwa muhimu sana kwenye uchaguzi wao ulioisha ni Shirika lao la Posta, yaani USPS.

Hii taasisi ambayo kwa miaka mingi iko hoi bin taaban kifedha, ilitegemewa sana kipindi hiki kutokana na janga la korona. Watu wengi sana walipiga kura zao kwa njia ya posta kama njia mojawapo ya kudhibiti maambukizi ya korona.

Trump alijaribu kupiga vita bila mafanikio utaratibu huu ambao umekuwepo miaka yote.

Katika video hii, gari la posta linashangiliwa baada ya kuonekana linapita mitaani.



Embu waza tu, wenzetu hadi shirika la posta linasimama kidete dhidi ya presha za Rais aliye madarakani na kuamua kusimama katika misingi ya kazi zao.

Huku sisi, taasisi zoooote za umma na za dola zinaona ni wajibu wao kupokea na kutekeleza hata amri haramu kisa tu zimetoka kwa Rais aliye madarakani.

Bado tuna safari ndefu sana.
 
Ingawa safari ni ndefu bado lakini jana sio leo.
Hata huko America hawajafika bado!
 
Hata kama wametutangulia na haya mambo ya demokrasia, ndio watuzidi hata kwenye kushangilia?

Maana huku Colombia matokeo yalivyotoka watu waliyapokea kwa sonona, hata walioshinda ilikuwa kama hawana furaha moyoni
 
Sidhani kama ni kusema wenzetu wako mbali sana kwa sababu ukisema hivyo inamaanisha tuko njiani na kwamba iko siku tutafika huko.

Lakini kiuhalisia ukweli ni kwamba hili ni swala la kiutamaduni zaidi. Sisi waafrika hatukuwa na chembe yoyote ya demokrasia katika mifumo yetu ya utawala na ndicho kinachokusumbua hadi leo.

Hatuamini katika haki ya wananchi kuchagua viongozi wanaowataka wao badala yake watawala wanaona hilo jukumu ni lao na kwamba wananchi ni watu wa kutawaliwa tu kibabe, hiyo ndio tofauti yetu na wazungu.
 
Ku engage wanaojaribu kuonyesha ulinganisho Kati yetu na wao ni kupoteza brain cells na muda.
 
Majitu ya kwetu huku hayajitambui! Tena naomba Magu ayahenyeshe kabisa haya mapolisi asiongeze mshahara kabisa, pumbavu! Aongeze mshahara pesa aitoe wapi wakati miradi mikubwa inahitaji pesa nyingi?
 
Back
Top Bottom