Video hii inayodaiwa ni Nkuruma Street, City Center jijini Dar-es-Salaam asubuhi ya leo, inahusu tukio gani?

Video hii inayodaiwa ni Nkuruma Street, City Center jijini Dar-es-Salaam asubuhi ya leo, inahusu tukio gani?

Wadau,kuna video inasambaa huko mitandaoni ikionyesha wahudumu wa afya katika mtaa unaotajwa ni mtaa wa Nkuruma street katika ya jiji asubuhi hii wakitoa kinachoonekana ni mwili wa mtu huku wakiwa wamevaa gloves na mavazi maalumu ya kuwakinga na maambukizi(protective gear).

Swali:kuna nini kimetokea kwa anaejua?

Wahusika tunaomba ufafanuzi.

Umeona maiti zinazookotwa huko New York na kutupwa kwenye malori kisha kwenda kuzikwa kwenye makaburi ya halaiki?
 
Kiingereza hujui halafu hiyo video imekuwa manipulated na wahuni ili kuichafua serikali yetu tukufu.

Sijui wameokota wapi hiyo video halafu mnawadanganya watu hapo ni Bongo
Kitu kichafu kinachafuliwaje tena?
 
Kiingereza hujui halafu hiyo video imekuwa manipulated na wahuni ili kuichafua serikali yetu tukufu.

Sijui wameokota wapi hiyo video halafu mnawadanganya watu hapo ni Bongo
Mtaaa wa nkuruma karibu na clock tower ndugu usibishe karibu tena na jengo la bora
 
Mna uhakika mnachongelea ndio kikichomo kwenye video? Mbona kwangu imefunguka video ya X?

Jr[emoji769]

Funika mdomo na pua kwa sehemu ya ndani ya kiwiko cha mkono unapopiga chafya.Kwa maelezo zaidi msikilize Ummy
 
Sio kweli. Video ni ya Tanzania. Angalia hata tangazo la bia ya serengeti, lugha inayozungumzwa, plate number za taxi na hiyo ambulance. Hapo hakuna manipulation.

Ila sina uhakika kama hao wanaookotwa ni sababu ya corona

Achakutuchota wewe..
Hizo plate no Umeziona wapiii..?!!
 
Funika mdomo na pua kwa sehemu ya ndani ya kiwiko cha mkono unapopiga chafya
Sawa nafunika, na wewe zuia muingiliano wa watu wa Jiji la Dar lililoathirika na COVID-19 na mikoa mingine isiyo na maambukizi - hili nalo hadi ufundishwe kaka!!
 
Back
Top Bottom