- Source #1
- View Source #1
Wakuu nimekutana na hii video inayoonesha familia ikiwa juu ya Mamba na vitu vyao kwenye mto, pia inadaiwa ni huko Goma, DRC. JamiiCheck naomba mtusaidie kupata uhalisia wa video hii.
- Tunachokijua
- Akili mnemba (AI) ni seti ya teknolojia zinazoiwezesha kompyuta kutekeleza majukumu mbalimbali ya kina na kwa uwezo mkubwa na haraka kadri ya maelekezo ya mtumiaji, ikiwa ni pamoja na uwezo wa kuona, kuelewa na kutafsiri lugha inayozungumzwa na maandishi, kuchanganua data, kutengeneza picha na video na kutoa mapendekezo ya utatuzi wa matatizo mbalimbali.
Kadri siku zinavyokwenda teknolojia hiyo imekuwa ikiimarika zaidi kutokana na maboresho ambayo yamekuwa yakifanyika ili kuendana na uhitaji na matumizi katika masuala mbalimbali. Pindi inapotumiwa vizuri na kwa mlengo chanya huwa na manufaa makubwa ikiwemo kuongeza ufanisi wa kazi na kadhalika. Aidha baadhi ya watu wasio na nia njema wamekuwa wakiitumia katika kupotosha taarifa mbalimbali katika Jamii.
Ni muhimu kila wakati kujifunza na kupata maarifa yanayowezesha kutambua maudhui ya picha, video, sauti na maandishi yaliyotengenezwa kwa kutumia teknolojia ya akili mnemba.
Kumekuwapo video inayosambaa mtandaoni ikionesha Familia ikiwa na mali zao juu ya mamba kwenye mto, ikidaiwa kuwa ni Goma, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Je ni upi uhalisia wa video?
Ufuatiliaji uliofanywa na JamiiCheck ulibaini kuwa video hiyo si halisi bali imetengenezwa kwa kutumia teknolojia ya akili mnemba.
Aidha JamiiCheck imebaini mapungufu kadhaa katika video hiyo yanayothibitisha kuwa video hiyo imetengenezwa na haiakisi uhalisia.
Sehemu ya mapungufu hayo ni pamoja na kukosekana kwa macho kwa watu wote wanaoonekana juu ya mamba. Uwepo mkono wa mwanaume aliyeshika fimbo, ambayo haitikisiki kulingana na mawimbi ya maji. Mkono ulioshikilia begi katika hali isiyo ya kawaida upande kushoto mwa picha ambao una vidole vinne na si vitano kama ilivyo kawaida.
Kifaa cha utambuzi wa maudhui yaliyotengenezwa kwa akili mnemba kwa kuainisha mapungufu katika sura za watu kinaainisha viashiria vya video hii kuwa imetengenezwa kwa teknolojia hiyo