SI KWELI Video hii ni Tembo akimuokoa chui kwenye kwenye mafuriko huko Indonesia

SI KWELI Video hii ni Tembo akimuokoa chui kwenye kwenye mafuriko huko Indonesia

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Source #1
View Source #1
Video imeripotiwa kuwa ni tukio lililotokea nchini Indonesia baada ya mafuriko makubwa ambapo tembo anaonekana akimuokoa Chui kutoka kwenye mafuriko hayo kitendo kilichovutia watu wengi.

Je, video hii ni halisi au imetengenezwa?




Screenshot_20251225-201859_Instagram.jpg
Screenshot_20251225-202353_Instagram.jpg
 
Tunachokijua
Mwishoni mwa mwezi Novemba 2025 yaliripotiwa mafuriko makubwa nchini Indonesia ambapo ripoti zinaeleza idadi kubwa ya waliofariki huku wengine wakipoteza makazi kutokana na mafuriko hayo.

Kutokana na mafuriko hayo ipo video iliyochapishwa mtandaoni na kueleza kuwa eneo la Sumatra nchini Indonesia, na kubainisha kuwa tukio la kugusa hisia za mamilioni ya watu duniani ikionesha tembo wa Sumatra akijaribu kumuokoa chui aliyekuwa amekwama kwenye maji ya mafuriko.

Je, tukio hili ni halisi? au video imetengenezwa?

Ufuatiliaji uliofanywa na JamiiCheck kwa kutumia nyenzo za kidigitali umejiridhisha kuwa video hiyo si halisi bali imetengenezwa kwa kutumia teknolojia ya Akili Unde.

Kadhalika miongoni mwa wadau walioshiriki kuthibitisha video hii wameeleza uwezo wa chui kuogelea kwenye maji na kwamba katika tukio hiloangeweza kujiokoa mwenyewe. Tovuti ya Tiger Safari India inaeleza kuwa chui ni miongoni mwa wanyama wanaoweza kuogelea kwenye maji na mara nyingi huweza kuvuka umbali mrefu majini.​

1767593095587-png.3525494
Mnamuuliza nani? Nyie si ndo wajuaji mjijibu 😏
 
Sauti ya mtiririko wa maji sio halisi. Haiendani na picha. Pia huo mkondo wa maji kwa mnyama kama tiger mbona ni kama chai na mkate tu.
 
Hiyo clip ni AI generated creation sio real event.
Wakati Tiger anaruka anaonekana ana mikia miwili.
 
Tiger ana mikia miwili halafu miwili halafu alivyolala kwenye mgongo wa tembo mkia uliangukia upande wa pili na bado huku ukaonekana.

Kingine mkondo wa maji unalia as if aliyerekodi yuko ndani ya hayo maji , wakati video inaonekana imechukuliwa mbali 😂
 
Hizi AI visdeos/picha zimekiwa balaa sasa! Uongo, uongo,uongo kila mahali!🤬 Wawe waungwana basi, wawe wanasema wazi kuwa ni AI
 
Hamna kazi hapo, lie. Chui anaingia mtoni na anakamata mamba wadogo na size ya kati na anatoka naye nje kwa haya maji sio kweli
 
Back
Top Bottom