- Source #1
- View Source #1
Video imeripotiwa kuwa ni tukio lililotokea nchini Indonesia baada ya mafuriko makubwa ambapo tembo anaonekana akimuokoa Chui kutoka kwenye mafuriko hayo kitendo kilichovutia watu wengi.
Je, video hii ni halisi au imetengenezwa?
Je, video hii ni halisi au imetengenezwa?
- Tunachokijua
- Mwishoni mwa mwezi Novemba 2025 yaliripotiwa mafuriko makubwa nchini Indonesia ambapo ripoti zinaeleza idadi kubwa ya waliofariki huku wengine wakipoteza makazi kutokana na mafuriko hayo.
Kutokana na mafuriko hayo ipo video iliyochapishwa mtandaoni na kueleza kuwa eneo la Sumatra nchini Indonesia, na kubainisha kuwa tukio la kugusa hisia za mamilioni ya watu duniani ikionesha tembo wa Sumatra akijaribu kumuokoa chui aliyekuwa amekwama kwenye maji ya mafuriko.
Je, tukio hili ni halisi? au video imetengenezwa?
Ufuatiliaji uliofanywa na JamiiCheck kwa kutumia nyenzo za kidigitali umejiridhisha kuwa video hiyo si halisi bali imetengenezwa kwa kutumia teknolojia ya Akili Unde.
Kadhalika miongoni mwa wadau walioshiriki kuthibitisha video hii wameeleza uwezo wa chui kuogelea kwenye maji na kwamba katika tukio hiloangeweza kujiokoa mwenyewe. Tovuti ya Tiger Safari India inaeleza kuwa chui ni miongoni mwa wanyama wanaoweza kuogelea kwenye maji na mara nyingi huweza kuvuka umbali mrefu majini.